Monday, October 10, 2016

Gomesa Tv

KAJALA- Ukiwa na sifa hizi njoo tuzae

Malkia wa muziki wa kizazi kipya Kajala Masanja, amesema kwa sasa yupo tayari kuzaa na kuongeza mtoto wa pili wa kiume endapo mwanamme atakuwa na sifa .Mwigizaji huyo ambaye ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Paula aliyezaa na prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’, amesema anahitaji Paula apate kaka yake.

“Najua mtoto ni mtoto lakini kwa sasa natamani kuwa na mtoto wa kiume ili Paula naye ajivunie kuwa na kaka. Siku zote nilitamani nipate watoto wenye jinsia tofauti na sasa tayari ninaye wa kike ni zamu ya kumpata mwingine wa kiume,” Kajala aliliambia gazeti la Mtanzania.


Aliongeza, “Natamani kuzaa na mwanaume yeyote aliye tayari na anayejitambua na kuwa tayari kuitwa baba na kugharamia matumizi ya watoto wangu na kuipa familia matunzo bora.”

Kwa upande mwingine, Kajala ameweka wazi kuwa anatamani kuvuka nje ya nchi kimafanikio, jambo ambalo tayari kwa sasa limeanza kuonesha dalili kwa kiasi kikubwa.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi