Thursday, October 29, 2015

Gomesa Tv

Prof Jay atamka maneno haya baada ya kushinda Ubunge

BAADA ya kuchaguliwa Ubunge, hii ndio kauli ya kwanza ya mwaasisi wa Muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, na sasa mbunge mtarajiwa wa jimbo la Mikumi huko Morogoro.

Naanza Kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma kwa kuniwezesha kufika mahali hapa nikiwa mzima na mwenye afya njema na kunipigania katika kila vikwazo na changamoto mbalimbali nilizopitia.

 Pili napenda kuwashukuru sana wananchi wote wa jimbo la langu MIKUMI kwa kuniamini, Kunichagua na kunipa Heshima hii ya kipekee na dhamana hii ya kuwatumikia, Nawaahidi nitashirikiana nanyi kwa unyenyekevu mkubwa, kwa nguvu zangu zote na uwezo wangu wote bila kujali itikadi za vyama vyetu, Maana Lengo letu kuu ni kuleta mabadiliko na maendeleo ili tuweze kuijenga MIKUMI tunayoitaka, 

Mwisho kabisa napenda kuwashukuru sana Ndugu, Jamaa na Marafiki zangu wote kwa kuonyesha Upendo na ushirikiano wa nguvu kwa namna moja ama nyingine mpaka kunifikisha hapa nilipo sasa... MIKUMI MPYA KWA MAENDELEO YA WATU WOTE! Mungu awabariki sana, ASANTENI SANA!!!! (MBUNGE WA MIKUMI) Mp JOSEPH HAULE...


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi