Friday, October 2, 2015

Gomesa Tv

Matukio 10 katika filamu ya Dogo Masai

(1) Filamu inasisimua sana kulingana na kisa na stori yake, lakini pia inachekesha sana kwa jinsi walishiriki walivyoigiza, yaani watu watu wenye tabia tofauti kuishi sehemu moja ni kazi kubwa sana, mmoja akiwa msomi (Dr) mwingine mvuta bangi na mwingine maisha bora.
(2) Filamu imetengenezwa na Timamu Effect Media ambao kwa upande wa rangi , picha inaonekana vizuri yaani usiku unajulikana huu ni usiku na mchana unakuwa ni mchana ule utofauti unaouna.
(3) Kitu cha tatu ambacho hukijui juu ya graphics katika filamu hii, wamefanikiwa kutengeneza mvua ya bandia ikafafa zaidi na mvua ya kweli, ni ubunifu wa hali ya juu inakuhitaji utulivu kugundua.
(4) Kingine katika make up, walifanikiwa sana pale mshika kamera Saidi Maghushi alipooonekana mbele ya kamera kama mzee wa miaka mingi kumbe ni kijana safi sana.
(5) Ambacho wengi hugoma sijui kwa nini, lakini katika filamu hii imetumia nyimbo za kwetu. Soundtrack aliyetengeneza naye yupo humo humo, ila angalie usitolewe machozi na wimbo wake.
(6) Zaidi ya filamu lakini kuna kipaji zaidi pale nyimbo kama Ni shida na Bora nirudi nyumbani zimetoka katika mkono wa mpiga gitaa na mdomo James Samale ambaye aliigiza kama rasta Samale ulinogesha zaidi filamu.
(7) Waigizaji walioendesha filamu nzima walikuwa wanne, Hissan Muya ‘Kitonsa’James Samale ‘rasta Samale’, Omary Clayton ‘James’ daktari Poul na wengine ni Mainda, Julieth Samson ‘Ummy’ ambaye aliigiza kama mama yake James.
(8) Kingine unakafurahia zaidi kukiona ni jinsi ya uchezaji wa muziki wa Bongo Fleva aliokuwa akiimba rasta, ukipokelewa na msomi Dokta, harafu ukichezwa na Dogo Mmsai.
(9) Kingine ambacho kipo katika filamu hii ni nchi, ilivyoweza kutwaa tuzo nchini Marekani, ila ukiangalia utangundua kwanini tuzo waliipata.
(10) Nifilamu ambayo inatoa funzo, kwani huwezi kumjua adui wako ni nani?
 — with Kemmy Julieth.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi