Sunday, September 13, 2015

Gomesa Tv

Wasanii waliojiunga na UKAWA waongezeka

WAKATI mbilingembilinge la wasanii kuchagua vyama, wasanii katika timu ya UKAWA imezidi kuongezeka kila kukicha.

Hivi sasa kuna wasanii ambao mara ya kwanza au hawakusika kama wapo lakini sasahivi wamejitokeza rasmi, akiwemo At, Rado,Timbulo,Bob Junior, Selemani Barafu, Niva, Makupa na wengine ambao kila kukicha wanazidi kuongezeaka.
huku kampeni zikiwa  zinaendelea vizuri katika kila upande na hata yale maneno yanayoongelewa ni utani kama ule uliop kwenye timu za mpira wa Yanga na Simba, changamoto kubwa iliyopo ni kwa wapiga kura kwa sababu wanatakiwa kuangalia sera muhimu kama afya na elimu kutoka kwa wagombea wao.
Kwangu naona muelekeo wa kampeni ni mzuri lakini tunaomba hali ya amani na utulivu iwe hivi hivi mpaka siku ya uchaguzi itakapofika ili tupate kuchagua viongozi sahihi watakaotuwakilishia matatizo yetu huko bungeni.
Muonekano wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu uko vizuri sana tu sema wanatuharibia wale watu wanaotumia muda huu kutoa kauli chafu zenye kuwakera watu badala ya kutangaza sera muhimu kwa wananchi kwa sababu wao ndiyo waamuzi.
Kampeni za mwaka huu ni tofauti na za miaka iliyopita kwa sababu  kuna muamko mkubwa kutoka kwa akina mama na vijana ambao wengi wao wana kiu ya kupata mabadiliko na hata idadi ya wapiga kura nayo inaonekana kuwa kubwa.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi