Saturday, September 5, 2015

Gomesa Tv

Wakata viuno Misri waendelea kukiona cha motoMahakama nchini Misri imewahukumu wanenguaji viuno wawili kufungwa jela miezi sita kila mmoja kwa kuchochea uasherati.

Suha Mohammed Ali na Dalia Kamal Youssef, wanaojulikana kama Shakira na Bardis wa Misri, walikamatwa kwa kusakata ngoma katika video wakiwa nusu uchi.
Mawakili waliwasilisha malalamishi kortini, wakisema wawili hao walikuwa kero kwa umma kimaadili na waliwaharibia sifa wanawake wa Misri.
Mwezi Machi, mchezaji densi mwingine kwa jina Safinaz alifungwa jela miezi sita kwa kuikosea heshima bendera ya taifa hilo.
Alikuwa ametokea kwenye video akivalia nguo yenye rangi za bendera ya Misri.
Msakataji densi mwingine, Salma el-Fouly, alifungwa miezi sita mwezi Julai kwa kucheza kwenye video akiwa amevalia mavazi mafupi na kuonekana kuchezea waume.
Mwanamume aliyepiga picha hizo za video pia alifungwa jela miezi sita, huku mwanamume wa pili aliyetokea kwenye video hiyo na ambaye pia alihudumu kama produsa akihukumiwa mwaka mmoja jela bila yeye kuwa kortini.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi