Thursday, September 3, 2015

Gomesa Tv

Siri ya mtoto Tiffah ni hii@Dimond asema.

·  Diamond Platnumz amesema mtoto wake Tiffah aliyezaa na mpenzi wake wa Uganda, Zari the Bosslady ni kama photocopy ya sura yake.
Akiongea kwenye kipindi kipya cha EFM Uhondo kinachoendeshwa na mtangazaji wa zamani wa Clouds FM, Dina Marious, Diamond alisema hana shaka kuwa Tiffah ni damu yake. “Unajua mtoto kama si wako ni rahisi tu kujua. Na unajua mzazi anakuwa mtu wa kwanza kugundua kama mtoto si wako,” alisema Diamond. “Tena wazazi wetu wa Kiswahili wanakuaga sijui na machale gani akiona kama anasema ‘baba copy sio yako.’ “Yaani Latti ukimuona kabisa utasema ‘huyo Platnumz’.
Kuhusu kauli ya mpambe wa ex wa Zari kuwa mtoto huyo si wa Diamond, muimbaji huyo wa ‘Nana’ alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakimchokonoa ile awajibu lakini bado hawezi kuwapa hiyo ‘pleasure’. “Mimi huwa nasema jamani nyinyi mnasema mna hela, matajiri mmeshamwacha mwanamke sasa mbona mmekuwa mnafuatilia?,” alihoji Diamond.

“Fanyeni shughuli zingine, mna hela tafuteni wanawake wengine wazuri zaidi yake mfanye vitu vingine. Still wanazidi kuniprovoke lakini haipendezi,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine Diamond alisema wanapanga kuwa na mtoto wa pili baadaye. “Mimi natamani kuwa na watoto wawili,” alisema. “Na yeye pia akasema ‘Latti akishakua kidogo tutafute mtoto mwingine, tumalize shughuli’, nikamwambia basi yaani hapo utakuwa umeniteka mazima mazima.”
Kuhusu ndoa, Diamond alisema ni kitu kinachoweza kufanyika mapema.
“Sijaona bado kuna kitu gani ambacho kitanifanya nichelewe.”
·
 

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi