Sunday, September 13, 2015

Gomesa Tv

Mahabusu Filamu iliyomtoa chozi JB kisa Kuambiana.

WAKATI filamu ya kampuni ya Jerusalem ikisubiriwa kwa hamu sana na mashabiki wa filamu kutoka katika kampni hiyo, inayomilikiwa na Jacob Steven ambayo tayari ilishatoka na filamu kali kama Chausiku, Wageni wangu, Zawadi na Mzee wa Swaga, kiongozi wa kampuni hiyo alijikuta akimwaga machozi baada ya kuona kava la filamu hiyo mpya.

Jb alisema alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa Blog hii, alisikita sana na kusema anamkumbuka sana marehemu Adam Kuambiana kwakuwa ndio alikuwa mtu wake wa karibu na kumshauri katika masuala ya filamu, na hata kumtumia katika kuongoza kwa baadhi ya filamu zake.
JB alisema kutoka kwa filamu ya Mahabusu kwake anaona ni sawa na kumuenzi mwigizaji huyo, lakini wakati akimalizia kauli hiyo chozi lilianza kumlenga lenga.

Haikuchukua muda machozi yalianza kumdondoka kuonesha ni jinsi gani alivyokuwa akiongea kwa hisia juu ya mwingizake mwenzake ambaye alifariki dunia mwishoni mwa mwaka jana.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi