Wednesday, September 23, 2015

Gomesa Tv

Baada ya kurudi Hija King Majuto ataigiza tena?

Kuna baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii, walimpongeza mwingizaji nguli wa filamu za kuchekesha King Majuto kwa kujitolea kwake kwenda kuhiji katika mji wa Makka na kuwa miongoni mwa mahujaji ambao wakirudi rasmi watatambulika kama alhaji Amri Athumani  au Alhaji King Majuto.


Hata hivyo mashabiki wengi hasa wa dini ya kiislamu wamekuwa wakijiuliza kwamba, kazi yake ambayo ya kuigiza na nafasi ambayo yupo sasa kama mfano wa kuigwa katika dini hiyo ya kiislam, Je ataendelea kuigiza na kushika viuno na wanawake au ataachana na kazi hiyo na kuutumikia kama alhaji?
Baadhi ya mashabiki wamempongeza kwamba huenda kwenda kuhiji ni kujitakasa kwa kile ambacho amekitumikia katika maisha yake, na lengo lake kwa sasa ni kutulia na kumsujudia mungu huku akiachana na kazi hiyo ingawa hadi sasa bado mwenyewe hajasema chochote kuhuju u - alhaji wake na kazi yake ya Sanaa.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi