Tuesday, August 25, 2015

Gomesa Tv

Denis azoa Mil 50 TMT

UKILALA masikini unaamka tajiri, ndivyo ilivyokuwa kwa mwigizaji chipukizi, Denis Lwasai, aliyewahi kufanyakazi na marehemu Steven Kanumba, baada ya usiku wa kuamkia jana kuibuka na kitita cha shilingi milioni 50 alizopata baada ya kuibuka mshindi katika shindano la Tanzania Movie Talent (TMT).

Katika shindano hilo, washiriki 10 waliingia fainali na kisha kuchezeshwa wawili wawili katika igizo lililokuwa likionyesha unyenyekevu wakati wa kuomba kazi. Hata hivyo, washiriki wote 10 wataigiza filamu itakayoandaliwa na kampuni iliyoandaa shindano hilo.

Pia katika fainali hiyo ambayo msanii Ruby alitumbuiza, wadau mbalimbali wa sanaa ya maigizo na filamu walitunukiwa vyeti vya shukrani kwa kuchangia ukuaji wa sanaa hiyo.

Visenti Kigosi ‘Ray’ alitunukiwa cheti cha uongozaji bora wa filamu, Ali Yakuti alipata cheti cha uandishi bora wa muswada (script) huku cheti cha mpiga picha bora kikienda kwa Christant Mhenga aliyekuwa akiongoza michezo ya maigizo ya mambo hayo miaka ya nyuma na cheti cha muongozaji bora wa michezo ya runinga alipewa Tuesday Mhangala aliyeongoza Jumba la Dhahabu.
Mtanzania

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi