Tuesday, August 25, 2015

Gomesa Tv

Alichoandika Diamond kwa wanaohama CCM.

Wakati Siasa ikiendelea kuumiza vichwa vya watu wengi huku wengine wakijielezea wazi wazi wapo chama gani, kwa kufanya safari fupi fupi za kutoka chama kimoja kwenda chama kingine. Mwanamuziki ambaye anacheza na anga za Kimataifa Diamond Platnumz au Baba Tiffah, ameandika haya kwenye mtandao wake wa Facebook.


Usipokuwa na Ufahamu mkubwa, leo unaweza dhani eti nna Maslahi Binafsi... ila siku Huu Uchaguzi utapopita ndio mtakumbuka Nilichokuwa napost Hapa... Hebu jiulize kwanini wao wakione Chama Kibovu leo baada ya kukatwa wao????? Mbona siku zote hawakuliona hili??? Kwakuwa Wamekosa ndio Ghafla Chama kibaya..???? Si juzi tu walikuwa wanakisifia???? Tena Masifa kedekede, baada wao kukosa ndio kimekuwa kibaya... Kama una FACT nijibu hapo ili mimi na wewe Tuijenge nchi yetu, Matusi hayatokusaidia wewe, Mimi wala Mtanzania Mwenzetu ataesoma hapa, Tuelekezane kibusara Ukinipa Point basi naja, Kama Hauna Point nakukaribisha....

Wakati huo mashabiki wake wameanza kumtaadharisha mwanamuziki huyo kuhusiana na siasa kwa maana itapotezea mashabiki wengi na kumpelekea kupotea katika ulimwengu wa muziki ingawa atapata fedha kwa kipindi hiki.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi