Wednesday, July 15, 2015

Gomesa Tv

Zanzibar International Film Festival (ZIFF) na Bongo Movies.
 HUENDA ikawa hii ni nafasi nyingine kwa wapenzi, waandaji na watizamaji wa filamu nchini kwenda kuhudhulia Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) ambalo linafanyika kila mwaka katika kisiwa cha Zanzibar na kutambulika zaidi kwa jina la tamasha la Majahazi .

ZIFF ni miongoni mwa  matamasha makubwa nchini huenda likawa kubwa zaidi kwakuwa linakutanisha wadau wa tasnia kutoka Afrika na Dunia kwa ujumla, huku likionesha filamu tofauti .
Lakini kikubwa lazima ifike tujiulize maswali baada ya  mwaka huu kuwa ni msimu wa 17,  tangu ilipoanzishwa kwake je!  inasaidia kukuza tasnia ya filamu Tanzania na kitu gani zaidi wasanii huwa wanakipata kutoka ZIFF.

Akizungumza na mwandishi wa safu hii hapa Bongo Unit, Meneja wa Tamasha la ZIFF, Danniel Nyalusi , amesema mwaka huu kidogo tasnia ya filamu za hapa Tanzania imejitahaidi kwa kiasi kikubwa ingawa si sana kuingingiza filamu zao katika tamasha hilo.

Alisema filamu ambazo zimewafikia kutoka Tanzania ni filamu 30, ambapo zimekaguliwa na kupatikana filamu 16 ambazo ndizo  zilizofanikiwa kuingia kuwania nafasi mbalimbali katika kipengele cha tuzo za  Zuku Bongo Movie .
Alizitaja miongoni mwa filamu ambazo zimeingia katika kipengele hicho ndani ya mabano ni mwongozaji wa filamu hiyo.

Filamu ya Mapenzi ya Mungu (Alex Sponga), Mr Kadabanja (Adam Kuambina), Fundi Selemala (Issa Mussa ‘Cloud 112’),  Mbwa Mwitu (Leah Mwandemseke), Dady’s Wedding  (Honeymoon Algebri), V.I.P (Vicent Kigosi), Single Ziro (Timoth Conrad), Pishu (Leah Mwendemseke), Samaki Mchangani (Amil Shivji), Kutakapokucha (Simon Mwakifamba), Msago (Haji Usi), Mikono Salama (Jacob Stephan), Nyange Kigoma (Saidi Hemed Ally), Going Bongo, Kilimo 2 na Faraja.

Nyalusi alisema pia zipo filamu tano, ambazo zimeingia kuwania nafasi za filamu za Kimataifa ambapo zamani wasanii wa Tanzania walikuwa wakiogopa kabisa kuwania nafasi hizo.
 

Filamu hizo ni Single Ziro (Timoth Conrad), Pishu (Leah Mwandamseke),Kutakapokucha (Simon Mwakifamba), Mr Kandabanja (Adam Kuambiana), Daddy’s Wedding (HoneyMoon Algebri).
Alisema filamu 16 kati ya 30 ndizo pekee zilizofanikiwa kuingia na filamu 14 zilishindwa kuwania tuzo hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wa filamu kukosa ubora na lingine filamu moja kuwa na sehemu mbili ‘part 1 na part 2’.

Alisema kulingana na soko la filamu Tanzania,  Dar es salaam peke yake kunazalishwa filamu zaidi ya 30 kwa mwezi mmoja tu, lakini filamu zilizoletwa  katika tuzo hizo ni 30 kwa mwaka mzima.
Anasema sababu inayopelekea kutoletwa kwa filamu hizo katika tamasha hilo, ambapo zaidi ya kuoneshwa au kutangazwa kwa filamu pia kunampelekea msanii kujulikana kimataifa.

Nyalusi anasema sababu kubwa kwamba wasanii wengi wamekuwa wameuza haki zao, hivyo kuepeleka filamu katika tamasha hilo, au lingine lolote wanaona ni sawa na kuitangaza kampuni ambayo tayari alishamalizana nayao katika malipo.

“Wasanii wanaamini hilo ni jukumu la kampuni katika kupeleka popote filamu hizo kwakuwa wao tayari walishalipwa na kuza haki zao,” alisema Nyalasu.
Anasema hata hivyo msanii kuuza haki yako sio kwamba ndio umeuza na jina la utengenezaji , hivyo tuzo ya mtayarishaji bora bado inarudi kwa msanii au mwigizaji bora jambo ambalo anawasihi wapeleke kazi hizo.

Alisema hata hivyo zaidi ya kujulikana yeye na kazi yake, lakini pia wanapata fulsa ya kukutana na waandaji na waigizaji wa Kimataifa ambao tayari dunia inawafahamu kutokana na kazi zao.

Anasema kwa mwaka huu atakuwepo mwigizaji mkongwe ambaye alivuma na filamu ya Sarafina ya Afrika kusini, Leleti Khumaro filamu ambayo ilikuwa ikizungumzia ukadamizaji juu ya Waafrika wa Afrika Kusini.

“Mwaka huu tumemleta yeye kwakuwa tunataka kuitambulisha Afrika zaidi hasa Pan Africa, ndio maana tukamchague yeye,” alisema.
Alisema hata hivyo walishawahi kuja wakali wengine ambao mchango wao katika soko la filamu la dunia ni mkubwa kama Danny Glover (2009) ambaye alifanya vizuri katika mfululizo wa filamu ya Leather Weapon akiwa na Mel Gibson na Jet Lee.
Wakawaleta tena Mario Van Peebles (2012) ambaye anatambulika zaidi katika filamu ya Solo, Danny Sheffer (2013 na 2014)  anayeigiza kama Mandela, na mwingine aliyefanya vizuri katika filamu iliyoitambulisha Brazir katika soko la dunia Leonald Lun- Kang kupitia filamu ya City of God.
Wasanii hao na waongozaji wa filamu sio kwamba wanakuja na kuondoka ila huwa wanatoa elimu katika madarasa ambayo huandaliwa kwaajili ya masomo kuhusiana na filamu.

“Wasanii wanapata mwaliko maalum kuhusiana na madarasa hayo, na wanapata elimu na hata kuwasiliana na wasanii hao kuhusu ni jinsi gani ya kufanya kazi,” alisema Danny.
Lakini Danny alisema nafasi hiyo imeendelea kuwepo kila kukicha na kuwavuta wasanii na waongozaji wakubwa, lakini kinachofanya tasnia ya filamu isifaidike ni kutokana na wasanii wake kuwa waoga wa kuongea ingawa lugha wamekuwa wakiijua.
Lakini mwisho kama mwandishi nilimaliza kwa kuongea na mwigizaji Vicenti Kigosi ‘Ray’, ambaye ni miongoni mwa wasanii zaidi kwamba alikuwa akiudhulia tamasha hilo pia ni mhudhuliaji nzuri wa madarasa ya elimu.

Akizungumza na mwandishi Ray alisema kweli wamekuwa wakipata fulsa kubwa ya kuwaona au kuwasiliana na waandaji wakubwa wa filamu duniani, lakini kitu ambacho kinashindwa kufanya nao kazi kunatokana na bajeti ya filamu za Tanzania.
Anasema wasanii wa kimataifa wanaamini bajeti ndogo ni shilingi milioni mia tano, lakini wao filamu wanauza kwa milioni 50 jambo ambalo linawafanya wawaogope waongozaji na wasanii wanaokuja katika matamasha hayo.
 
“Tunaishia kupata elimu katika madarasa ambayo wanatoa elimu, na tunashukuru mungu inatusaidia lakini lakini bajeti yetu hairuhusu sisi kufanya kazi nao,” alisema.
Alisema pia anakubaliana na kwamba filamu nyingi huingia sokoni kila siku kiasi cha kufikia 30 kwa mwezi, lakini anasema filamu nyingi zinazoingia zinatokana na kila mtu kutaka kuwa mtayarishaji na sio mwingizaji.

Anasema hali hiyo inapelekea kila mtu kuzalisha filamu yake baada ya kuwa mwigizaji, hii inatokana na makampuni kulipa kiasi kidogo ndio maana mtu anaona ni bora kuzalisha filamu yake.
“Ndio maana filamu zinaingia sokoni zaidi ya 3o, lakini hakuna hata moja yenye ubora hali inayopelekea soko la filamu kuyumba kwa maana watu wanasema zote ni mbovu kutokana na chache walizoziona,” alisema.
Mwisho

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi