Saturday, August 2, 2014

Gomesa Tv

RIYAMA filamu ya Riyama Ally @ FILM REVIEW
 Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuona baadhi ya sehemu ya katika filamu ya Riyama, filamu iliyoandikwa na kuigizwa na mwigizaji Riyama Ally.

Kitu ambacho nimekipenda kwanza ni jinsi alivyoanza kusimama yeye kama yeye baada ya kuigiza filamu nyingi za watu, huku akisimama vizuri katika filamu hizo.
Kisha turudi kwenye kawaida yetu,  hasa kuhusu filamu hii ambayo inaingia sokoni hivi karibuni, chini ya kampuni ya usambazaji ya Pilipili Enterment.
Riyama Ally anasema  filamu yake ya Riyama ilikuwa ni filamu yake ya tatu, tangu alipoanza kuandika lakini zingine aliziuza , lakini hii pekee ndiyo aliyoamua kuisimamia na kuhakikisha anaikamilisisha chini na kuingiza sokoni.
Katika filamu hii ambayo nikipata nafasi nitaitizama tena,  kilichonivutia zaidi  katika filamu hii ni jinsi ilivyokuwa  makini katika  matukio na mtiririko wa kueleweka.
Pia waigizaji wake hawakuwa na pupa ya kuigiza yaani walikuwa wapo makini na kile walichokuwa wakikifanya, yaani Cast yake ilikuwa sahihi kwa kila mtu aliyeweza kushika nafasi yake.
Waigizaji kama Angel John, Omary Othamani, Mohamedi Likulo na Rihama mwenyewe waliweza kuonesha kiwango cha kizuri ingawa wapo walioonekana kama wachanga katika baadhi ya sehemu .
Filamu yenyewe inakisa chenye kuleta maswali mengi juu ya maswali, hasa kwa jinsi watu walivyoweza kuishi wakiwa wapenzi hadi mke na mume, huku mmoja akiwa ameathirika na na mwingine akiwa mzima.
Miongoni mwa maswali ambayo utakuwa ukijiuliza ndani ya filamu hii, ni jinsi mtu anavyoweza kuambukizwa virusi vya ukimwi bila ya kujamiana.
Huku  mwingine kukubali kuyatoa maisha yake kwa mtu anayempenda kwa kukubali kuishi naye ingawa alijua ni mwathirika wa ugonjwa huo.
Labda ningekusimulia kidogo juu ya filamu hii, inayozungumzia msichana anayeitwa Riyamaa.
Filamu inamsimulia Rihama kama msichana ambaye katika maisha yake ya usichana hakuwahi kufanya mapenzi na mwanaume yeyote na kuishi kama bikra.
Lakini alipoamua kujikita katika ulimwengu wa mapenzi, anagundua kuna tatizo ambalo mwanza hakujua nini hasa chanzo cha tatizo lake.
Katika hali ya kushangaza Riyama anakuja kugundulika ni mwathirika wa virusi vyinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi ‘HIV’.

Hali  hiyo inamkosesha amani na  kutamani kuishi peke yake, lakini mpenzi wake anampa na moyo na kumwambia sio mwisho wa maisha huku akimpa ahadi ya kuendelea kubaki naye .
Hapo ndipo linapokuja jambo la kushangaa , baada ya Mohamed  Likulo alipoamua kukata mzizi  wa fitina kwa kuanzisha familia na binti huyo, na hatmaye kupata mtoto.
Nilipomuuliza Riyama juu ya simulizi hiyo, alisema Kikubwa zaidi alichokuwa akikilenga katika filamu hii, ni kuielimisha jamii  kwamba kuathirika si kwamba ndio mwisho wa maisha.
Yaani sio kwamba ndio hutoweza kufanya lolote kwenye dunia hii, kwakuwa umeathirika.
Matukio ndani ya filamu mengi yameweza weza pia kuleta changamoto kwa mwandishi wa stori, kwani yapo ambayo yamekuwa kama yakivuruga mtu asijue nini kinaendelea.
Kikubwa Riyama amejaribu kutumia jina lake la Riyama, katika filamu hii kuonesha kwamba  anaweza kufanya vitu tofauti unaweza kuwa mwathirika na bado ukaweza kupata mtoto aliyekuwa salama.
Kuhusu picha Cameraman amejitahidi kuhakikisha picha inatoka nzuri, labda nitakapopata muda wa kuangali vizuri nitaweza kutoa makosa zaidi ya filamu yenyewe.
Mtu aliyekuwa akichagua Cast,  kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kwani wahusika waliweza kushabiana vizuri sana na nafasi zao, na kila mmoja alionesha uweza wake.
Lakini kwenye stori nilipenda sana kumsifia alijitahidi kuhakikisha filamu inakuwa tofauti na ndio jambo ambalo kwa sasa linahitajika kufanyika.
Mwisho


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi