Saturday, August 2, 2014

Gomesa Tv

NAJUA UPO BIZE@ Ila soma japo kidogo kuujua ugonjwa wa EBOLA kiundani zaidi.


Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na homa ya ubongo, na ni moja ya magonjwa yanayotishia uhai wa binadamu.Ugonjwa huu ulijulikana kwa mara ya kwanza, barani Africa mnamo miaka ya 1970 na mpaka sasa ugonjwa huu umeua zaidi ya watu 1,500.

Historia inaonesha Ebola imeua watu kwa asilimia 90, madaktari wameripoti kua ugonjwa huu umekua “tishio kwa binadamu”.

Dalili
Wengi wao wanaopatwa na virusi hivi vya ebola hupata:
1. Dalili kama za mafua
2. Homa
3. Uchovu wa ndani ya mwili
4. Misuli kuuma
5. Kichwa kuuma
6. Koo kuvimba.

Baadae muathirika huanza:
1. Kutapika
2. Kuharisha
3. Kupata upele
4. Ini na figo kutofanya kazi vizuri
5. Kuvuja damu ndani ya mwili
6. Kutokwa na damu kwenye tundu za mwili Mfano; macho,puani nk.
 
MUHIMU KUTAMBUA
Ugojnwa huu hauna tiba, yani kwa maana toka ugundulike miaka ya 1970 haujapata tiba mpaka hivi sasa.

USAMBAAJI WAKE
Ugonjwa huu upo kwa pande zote mbili kwa maana ya binadamu na wanyama na husambaa kwa njia kugusa damu ilioathirika, au majimaji, kidonda kilochoathilika.

Aidha, katika mazishi mengi ya kiAfrica wafiwa hua na tamaduni ya kuaga mwili wa marehemu kwa kuugusa, hii ni njia kubwa sana ya kusambaa kwa ugonjwa huu, kwani huu ugojwa unaishi hata kwenye mizoga ya wanyama na maiti za binadamu. Tafiti zinasema kuna aina ya popo wapo Africa wanabeba virusi hivi, popo hawa hula matunda mbalimbali, na pia huliwa na wanyama mbali mbali, kwa njia hii maambukizi ya ugonjwa huu unaweza kua mkubwa zaidi.

Mnamo mwaka 1976 Ebola iligundulika ghafla mara mbili katika nchi ya Sudan na Demokrasia ya Congo (DRC). Mlipuko huo wa ebola nchini DRC ulikua katika mto Ebola, ambapo ugonjwa huo ulipata jina hapo.
Mpaka sasa zaidi ya watu 1500 kutoka maeneo mbali mbali mwa bara la Africa washapoteza maisha kutokana na ugojwa huu.
Mungu atulinde Tanzania na ugonjwa huu, Mungu atuepushie Africa na Janga hili.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi