Saturday, August 2, 2014

Gomesa Tv

Hii ndio zawadi ya Kuambiana kwa Wiliam Mtitu
Huenda ukawa hujui lakini nguli wa filamu nchini, Wiliam Mtitu alikuwa akimtegemea sana mwigizaji Adam kuambiana katika kazi zake za sanaa,
na kabla ya kifo chake alimwacha wakati ameikamilisha filamu , ambayo kwa Mtitu anahisi kama ni zawadi ya mwisho.

Aliiambia Bongo Unit kwamba  Stupid Father iliongozwa na kuchezwa na Kuambiana,  ikafanya vizuri sokoni lakini kabla ya kufariki alishakamilisha filamu nyingine ya Who is  My Child.

Alisema filamu hiyo ameamua kuingiza sokoni muda huu kama kumuenzi, rafiki yake huyo na mfanyakazi mwenzake.
“Hakuna kama Kuambiana katika kampuni yangu, bado pengo lake litakuwa kubwa sana” alisema.

Mtitu alisema tangu alipoondoka Kuambiana hadi leo amekuwa akiangaika kumpata Mwongozaji mzuri atakayeweza kuongoza filamu zake kama ilivyokuwa kwa msanii huyo.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi