Monday, July 28, 2014

Gomesa Tv

Wasanii waendelea kupata Semina ya PSPF

Mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Mangele ‘Steve Nyerere’ amewataka wasanii wa filamu na muziki kujiunga na mfuko kuweka kwa hiyari wa PSPF ili kuepuka kuomba misaada wanapopata matatizo.

Akizungumza jana katika semina iliyoandaliwa na mfuko huo wa kijamii, alisema wasanii wengi wamekuwa wakifanyakazi bila ya kuwa na chochote ambacho kitawasaidia pindi wanapata  matatizo ikiwemo maradhi au hajari.
Alisema wanakuwa katika wakati mgumu wakati wa  kuchangishana, jambo ambalo si zuri kutokana na hali kuwa ngumu kwa sasa.

(Mwigizaji Simon Mwapangate 'Rado' akiwa na Zuberi Mohamed 'Rado')Aliwataka  kujiunga katika mfuko huo, ambao utasaidia kutatua matatizo yanayowakabiri pindi yanapotokea  na kupunguza tatizo la kuchangishana mara kwa mara.
“Sisi wenyewe mashahidi wenzetu wameugua na wengine kupata matatizo makubwa hadi kupelekea kifo, tumekuwa tukijikamua kwa kiasi kikubwa ili kusaidia. Ni bora tujiunge na mfuko huu ili tuweze kusaidiana pale  tunapopaweza,” alisema Mangele.
Naye mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Adam Mayinda alisema, mfuko huo zamani ulikuwa ukijishughulisha na taasisi za Kiserikali na Waajiriwa wa makampuni makubwa.
Alisema lakini sasa wameamua kutoa huduma hiyo kwa kila mtu, ili kuweza kunufaika kipindi cha matatizo au pindi anapokwama au anapohitaji fedha zake kwaajili ya jambo fulani.

(Fatuma Makongoro 'Bi Mwenda)


Alisema mtu anaweza kujitoa katika mfuko huo,  kulipwa kiasi chake chote alichoweka bila ya kukatwa kiasi chochote.
“Sisi hatufanyi biashara ila tunajaribu kuwasaidia watu kuweza kuhifadhi fedha zao,” alisema Mayimba.
Alifafanua zaidi kwa kusema mtu anaweza kujiunga kwa jia ya simu, pia akatuma fedha zake popote kwa njia ya simu na hata kuangalia taarifa zake kupitia simu yake ya mkononi.

Jenifer Kyaka 'Odama'
Vyonne Sherry 'Monalisa'
MtunisGomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi