Wednesday, January 8, 2014

Gomesa Tv

MAKALA; Weusi na mikakati mipya ya 2014

 
Tatizo la wasanii wa muziki wa kizazi kipya, hususani wale wa muziki wa Hip Hop, kulalamika kuibiwa kazi zao ingawa kudai kwamba kazi zao ni nzuri na  kumewapelekea wasanii wa makundi mawili kuungana ili kufanya kazi zao pamoja.

Makundi hayo kutoka mkoani Arusha, moja likitambulika kama Nako 2 Nako lenye makazi yako Ololo au Kololeni, ambapo mwanzo lilikuwa likiundwa na Ibra De Hustler , Isic Maputo ‘Lord eyes’, George Sextus ‘G Nako’ na wengine.
Wakaungana na kundi la Liver Camp, ambalo lenye makazi yake Daraja mbili likiundwa na ndugu wawili Dickson Simon’Niki wa pili’, na John Simon ‘Joh Makini’.

Kuungana kwa makundi hayo mawili, ndipo likazuka kundi jipya ambalo kwa sasa ndilo kundi ambalo linafanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kitika mtindo wa Hip Hop.
Akizungumza mmoja wa kundi hilo George Sextus ‘G Nako’, amesema kwa sasa kundi hilo linawasanii watano, akiwa Lord Eyes, Nikki wa Pili, Joh Makini na  Bonta.

Anasema kuungana kwa makundi hayo na kutokea kwa kundi hilo,  ni kukusanya nguvu ili kuweza kukabiliana na matatizo ambalo yamekuwa yakiwakuta wanamuziki wa Hip Hop.
Akizungumzia kuhusu matamasha, alisema kwa sasa tayari wameshaanzisha kampuni ambalo imesajiliwa kwa jina la Weusi, huku wakiandaa matamasha yao wenyewe.

“Sasa hivi tumekuwa tukiandaa matamasha yetu, na kila kitu tunafanya wenyewe” anasema.
Anasema katika kuandaa matamasha huwa wanakutana na changamoto nyingi, kuotokana na makampuni mengi yamekuwa yanasua sua juu ya kuwaunga mkono.
Hivyo kutokana na makampuni hayo kutokuwa na ushirikiano wa moja kwa moja, wamejikuta wakiandaa kwa fedha kutoka mfukoni mwao.
 


G Nako anasema changamoto nyingi katika kuandaa tamasha, huwa wanakumbwa na wasi wasi sana, kama fedha zao zitarudi au laa  hasa kutokana na kila kitu kutoka kwenye mikono yao.

“Ujue kuandaa kitu kwa fedha zako kuna hitaji moyo, kwakuwa unakuwa unawekeza fedha nyingi tatizo lipo karika kurejea kwa fedha hizo” anasema.
Kuhusiana na matatizo la wasanii wengi wa Hip Hop kulalamika nyimbo kutopewa kipaumbile kama muziki mwingine.

G Nako anasema umeshapita muda wa kulalamika, ilimradi kila msanii ajue njia gani azitumie ili kazi yake ifike kirahisi kwenye vyombo vay habari.
“Muda wa kulalamika umeisha, kila mtu anajua ni jinsi h=gani ya kufikisha kazi zake kwenye vyombo vya habari na kupigwa kwa kazi zao” anasema.
Anasema wao kazi zao zimekuwa zikipigwa bila ya wasi wasi kwakuwa wamekuwa wanafanya kazi nzuri.
Pia msanii huyo amesema katika kampuni hiyo, ya weusi kwa sasa wanatengeneza T-shit ambazo wanasambaza kupitia maduka makubwa ya nguo, na zingine wanasambaza kwenye vyuo ambapo wanamashabiki wengi.
“Huwa tunawauzia jumla watu wenye maduka makubwa na wao wanauza kwa bei wanazotaka wao, popote pale” anasema.
Zaidi ya T-shit anasema kwa sasa kampuni hiyo, imeshaanza kujipanga kutengeneza, kofia, soksi, boksa na nguo zingine kwaajili ya kuzisambaza zaidi kila sehemu.
Anasema lengo lao kwa sasa kampuni hiyo kuweza kuitanua na kufanya vitu vinyi, na sio kutegemea muziki kwa kila kitu, kwakuwa mziki wenyewe unaenda na kubadilika.
Kuhususiana na watu ambao wamekuwa wakidhamini kutengeneza kazi zao, kama muziki na video ambazo kwa sasa ‘zimekuwa na ghalamaku bwa.
G nako alisema kupitia kampuni yao, wamekuwa wakisaidiana  sana kuandika nyimbo, na huwa wanapeana nafasi ya kutoa wimbo jambo ambalo linawafanya waendelee kubaki kileleni kwa muda mrefu.
Hivyo amesema hata video zao, pia huwa wanashirikiana kufanya moja baada ya nyingine na kukamilisha kwa muda muafaka.
“Huwa tunasaidiana na washikaji katika kukamilisha video zetu, lakini kwa kiasi kikubwa sana wausika tunakuwa wenyewe” anasema.
Anasema kwa sasa kampuni yao inaandaa video nne,  mbili  wanafanyia  Arusha na mtayarishaji Nisha, ambapo kwa sasa wapokwenye hatua za mwisho.
Anasem baada ya hapo wanatarajia kufanya video ya wimbo  Bei ya mkaa, ambapo watafanya na Adam Juma wa Next level.
“Video ya mbili zingine ikiwemo Nikumbatie, ingawa bado hatujajua tutafanya na nani, ila nategemea mtayarishaji atatoka nje” alisistiza G Nano.
G nako anasema kupitia kampuni yao ya Weusi anasema, wamekuwa wakijiepusha sana na mabifu, au ugfonvi ambao kwao hauna tija.
Ugonvi anasema ndio umekuwa ukirudisha nyuma muziki wao, na hata wale wanaousikiliza wanaona kama wote wahuni na ndiyo maana hata mara kwanza walikuwa na vikwanzo vyingi kwa wazazi.
Anasema kwa sasa kampuni yao itaendelea kusimamia matamashao yao, na kuangalia vyanzo vingine vya mapato ikiwemo milio ya simu maarufu kama Ring tone.
Anasema kuhusu mgogoro wa ringtone, unakuja kutokana na wasanii wanafanya kazi kubwa lakini wanunuzi wa ring tone wanachukua fedha nyingi sana.
“Biashara ya Ringtone inatoka sana watu wananunua, lakini tukija kwenye kugawanya fedha zilizopatikana wao wanachukua mapato mengi, na ukiwauliza watakuambia kuna vijikato vidogo vido kama kodi na vingine” aliendelea kuelezea G Nako.
Katika suala zima la kuuza ringtone, anasema mwaka huu watahakikisha wanalikalia chini na kujaribu kujadili kama wataweza kukukbaliana, kwakuwa makato mengine anasema kwao hayana maana.
G nako anasema katika mwezi huu anatarajia mwezi huu, wanatarajia kufanya kazi nyingi kwa kila msanii, lakini ikianza yake akimshirikisha Lord Eyes na mzee Kiki.
Mwisho


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi