Wednesday, January 15, 2014

Gomesa Tv

Hivyo ndivyo ilivyotokea Bongo MovieWasanii wa kundi la Bongo Movies majuzi wamechagua viongozi wapya, ambao watakaoongoza kwa muda wa mwaka mmoja, huku wakiwa na malengo ya kuifanya taasisi hiyo kuweza kutanuka zaidi.

Kiongozi ambaye kwa sasa amechukua nafasi ya mwenyekiti  Steve Mangele ‘Steve  Nyerere’ akisaidiwa na Muhusin Awadhi ‘Dr Cheni’  kama mwenyekiti msaidizi, katibu au mtendaji mkuu nafasi iliyochukuliwa na William mtitu, makamu wa katibu Devota Mbaga.
Nafasi ya Hazina imeshikwa na Issa Mussa ‘Cloud 112’ huku akisaidiwa na Sabrina Lupia ‘Cath Lupia’ nafasi ambayo mara kwa mara imekuwa na mgogoro mkubwa.
Viongozi walioingia katika awamu hii, wengi walikuwa hawana wapinzani kwakuwa waliokuwa wapinzani walijitoa akiwemo, Hisani Muya, na hivyo walijikuta wakisimama mmoja mmoja, jambo ambalo wakapitisha mtu atakayekatailiwa kwa nusu ya kula basi  atakuwa ameshindwa uchaguzi huo.

Makubaliano hayo yalipelekea wagombea hao kujikuta katika wakati mgumu,  wapiga kura walikuwa 47, na kura zilikwenda Cath Lupia, alipata kura 41, 3 ziliharibika na 3, zilimkataa, Cloud 112 alipata 46 na mmoja iliharibika, William Mtitu kura 33, akichuana na Wastara Juma aliyepata kura 13 na mmoja iliharibika.
Dokta Cheni alipata kura 41 tano zilimkataa na mmoja iliharibika, wakati Steve Nyerere alipata kura 40 tatu zilimkataa na nne ziliharibika.


Hata hivyo Sela mbalimbali zilitangazwa katika kuwania vyeo hivyo, nahata wagombea walichemshana kwa kuongea wazi kwamba hawezi kufanya kazi na mtu fulani kulingana na sera zake, ingawa sera kwa upande mwingine watu walizipenda.
Miongoni mwa sera ambayo ilipendwa na wengi, ikawa kama sehemu ya kushangilia, ni ile ya William Mtitu, mtu ambaye anasifika kwa umakini na ukali wa hali ya juu alipotangaza.
Watu walipomuuliza kuhusiana na hasira zake, na jinsi alivyoweza kumpeleka msanii mwenzake polisi jambo ambalo alilijibu kwa kujiamini na kusema.
“Kama mnataka kunipa kura nipeni, lakini kama mnahisi viongozi wataiba mali ya Bongo Movie, huku mimi naona nikiwa kama mtendaji mkuu basi lazima niwapeleke polisi. Suala la suruhisho tutasuruhishana lakini suala la wizi lazima wafike polisi,” alisema Mtitu.
Kutokana na sera hiyo, alijikuta akipata ufuasi wa watu wengi ambao wengi wao waliokuwa wakilalamika, wapi fedha zilipoenda zile za mara kwanza.
Sera iliyokuwa ikitikisa na lilikuwa tumaini kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie, ni ile ya Steve Nyerere ya kuanza kugomea, fedha chache wanalipwa watengenezaji filamu.
Hata alisema lazima aitishe mkutano mkubwa wa watengenezaji filamu nchini, na wasambazaji ili kujua ni jinsi gani wasanii wanavyoweza kurekebishiwa haki zao na hata kutouza haki miliki.

“Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kugoma na mimi nitakuwa mtu wa kwanza kufokea, pale msanii atakapoonewa kwa hali yoyote kwa kuuza haki zake” Steve Nyerere alisisitiza.
Pia alisema miongoni mwa sera zake ni kuita Bodi ya wazamini, ambayo atakusanya matajiri mbalimbali ambao wataweza kuja kudhamini Bongo Movies, na hata kufanya mechi au michezo ya ghalama kwaajili ya kuchaza mfuko wao.
Hata hivyo kikubwa kilichowapa tumaini kwa wasanii wa filamu juu ya kauli ya mwenyekiti huyo mpya, pale alipokuja kuchukua fomu ya uongozi akisindikizwa na msafara wa matajili wanaouza magari mjini na watu maarufu.
Mikakati mbalimbali ambayo kwa sasa ndiyo tumaini la wasanii wengi wa Bongo Movie, ilipo ni juu ya mipango mipya kwa wasanii wote.
Miongoni ya mipango hiyo, ni kujenga ofisi ya Bongo Movie ambayo itakuwa maalum kwaajili ya wasanii kukutaniana hapo na kuendesha mikutano yao.
“Mimi na nyinyi tutashirikiana kuhakikisha tunapata eneo zuri la Ofisi, ambapo tutakuwa pia tukifanya mikutano yetu” alisema Steva.
Pia walipanga kufungua akauti ya benki ya Bongo Movie, ambayo haikufunguliwa tangu ilipoanza kwa taasisi hiyo.
Wanasema akauti ya benki itakuwa ikifunguliwa na watu , ambao ndio watakuwa wakisaini juu ya utokaji wa fedha, akiwa mweka hazina msaidizi, katibu na mwenyekiti wake.
Mikakati mingine waliyoipanga ni kuhakikisha safari za mikoani au za kimichezo, anakwenda mtu yoyote ambaye mwanachama na sio kwenda mtu kulingana na umaarufu wake, wakati kwenye vikao haudhulii.
Hata hivyo wapo pia waliolalamika kutochezeshwa katika filamu jambo ambalo nalo walisema lazima kila anayetengeneza filamu kutoka katika chama hicho achukue wasanii kuanzia watutu na kuendelea kutoka humo humo.
Miongoni mwa changamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wasaniii wengi, hasa kutoka katika uongozi uliopita wa Visent Kigosi, na kuamini huenda ukaendelea hadi katika uongozi huu mpya.
Changamoto hizo ni wasanii kuchukuana katika safari za mikoani, wakiwa wawili waili yaani wenye uhusiano jambo ambalo, wengi hawakulitaka kulijibu kama lilivyotakiwa na kulikwepa.

Swali lingine ambalo lilikuwa na mjadala mkubwa ni kuhusiana na kuliwa kwa fedha za michezo ambazo zilipita, kama za Mpira wa Miguu, na Net ball, ambazo hadi leo wanadai hawajui zilipo.
Changamoto kubwa nyingine ambayo uongozi wanakumbana nayo, ni kuhusu mpasuko wa wasaniii wakubwa kuwa na makundi, ambayo mara nyingi yamekuwa yakisababisha kudumaa na kutaka kufa kwa taasisi hiyo.
Hata hivyo mwisho wa siku uongozi mpya umesema yaliyopita si ndwele, tugange yajayo  baada ya kila mmoja kukiri kwamba alitenda makosa kwenye uongozi wake.
“Mimi nawashauri uongozi ujao, wasifanye kama yale tuliofanya katika uongozi wetu. Watu tulikuwa tukijadiliana na wengine walikuwa wakienda kuongea nje na kusema juu ya kile tulichopanga. Ni mara nyingi ubaya wote ulirudi kwangu” alisema Vicent Kigosi ‘Ray’ Mwenyekiti aliyemaliza uongozi wake.
Bongo Movie Unit ilianzishwa mwaka 2011, ikiwa chini ya watu watatu akiwa Jimmy Mafufu,  Captu Radon a Ben Kinyaiya.
Baada ya hapo waliaamua kuifikisha kwa watu wengine, ambapo ikaungana na kuwa ya watu tisa, chini ya uongozi wa Athuman Mbilinyi, akiwa mwenyekiti, na makamu wake Jacob Stephan, katibu Ben Kinyaiya makamu Captu Rado, mtunza hazina Single Mtambilike, msaidizi wake Vicenti Kigosi.
Mwaka 2012 Uongozi ukaja ukabadilika baada ya uchaguzi na Mwenyekiti akawa Jacob Stephan ‘Jb’, makamu Athuman Mbilinyi, katibu Cloud 112, makamu Jackline Wolper, mweka hazina Single Mtambalike na msaidizi wake Vicent Kigosi.
Mwaka 2013 viongozi  Vincent Kigosi aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mkuu, Irene Uwoya -Makamu wa Mwenyekiti , Chiki Mchoma Katibu Mkuu, Single Mtambalike aka Richie Richie alichaguliwa kuwa Mtunza Fedha Mkuu na Makamu wake kuwa Jackline Wolper.
Mwisho

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi