Monday, December 2, 2013

Gomesa Tv

Shabiki wa Yanga akutana na Dr Cheni na mchina wa Bss@ katika filamu NIMEKUBALI KUOLEWA

 
 
BAADA  ya kuingia sokoni kwa filamu ya Hukumu Yangu, mwigizaji  Muksin Awadhi ‘Dr Cheni’ aamua kumshirikisha Shabaki wa yanga Steven Mwamwala  na mchina maarufu aliyeshiriki katika shindano la Bongo Star Search.

Akizungumza na Bongo Unit, alisema amewashirikisha katika filamu yake  mpya, ambayo itaitwa Nimekubali Kuolewa, ambayo anaamini italeta mabadiliko katika tasnia nzima.

Akimzungumiza shabiki wa Yanga, ambaye  alipata umaarufu mkubwa kwa kulia baada ya timu ya Yanga kufungwa 5 bila na Simba, ameona ni bora kumtumia ili kuongeza radha kwenye filamu yake hiyo.

“Najaribu kuongeza radha ambayo watu wamekuwa wakiikosa, sio kila siku nije kitu kimoja kile kile na waigizaji wale wale” alisema.
Filamu ya Hukumu yangu imeingia sokoni, wiki hii baada ya kutangazwa sana na watu kuisubiri kwa hamu.
 
Steven Mwamwala aliyelia baada ya yanga kufungwa na ya kufungwa 0-5 na Simba

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi