Thursday, December 12, 2013

Gomesa Tv

Mzee Small azushiwa kifo mara ya pili

 
Ni mastaa zaidi ya 10 wa Tanzania ambao wamezushiwa kifo ndani ya mwaka 2013 na stori zote zikawa za uongo baadae, miongoni mwao ni Mwasiti na Mr Blue….. sasa December 10 2013 kuanzia saa nne usiku taarifa zilezile za kuzushiwa kifo zimemuangukia mwigizaji mzee Small ambae ni kweli kwa kipindi kirefu amekua akiugua.
 Bado yuko hai ila ana maumivu ya bega na mkono kutokana na mshtuko alioupata toka May 2012, Anasema ‘mlitaka kwenda kuchukua jeneza kutokana na taarifa za kifo cha uongo lakini sasa msichukue, hiyo pesa ya sanda hiyo mchukue mkanunulie watoto chakula wale.

 Usingizi wao usiku wa kuamkia leo December 11 2013 ulikua wa tabu sana, wamepigiwa simu zaidi ya 10 za watu mbalimbali hata usiku wa manane wakitaka kujua ukweli wa taarifa za kifo,  Familia ya Mzee Small inakiri hii ni mara ya pili kwa mwigizaji huyu kuzushiwa kifo ila ya mara hii ndio imekua kubwa kuliko.

 Mzee Small anasema ‘misaada ya Watanzania kwa njia mbili kaka, kwanza dua zao ndio maana sikufa… mimi sijafa bwana, mimi mzima kabisa, nawashukuru Watanzania.


 

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi