Monday, December 23, 2013

Gomesa Tv

Mwaka mmoja Bongo Movie mikononi mwa Ray@ Wanachama hoi

 
Baada ya mwaka mmoja kupita tangu Vicent Kigosi maarufu kama Ray, kuchukua madaraka katika Taasisi au kampuni ya Bongo Movie Unit, mambo yamekuwa tofauti na wanachama wake walivyotegemea.
Katika kikao kilichoitishwa na  kamati ya Uchaguzi ya Bongo Movie, chini ya mwenyekiti wake Mr Mafufu, alisema tangu walipomchagua mkali huyo wa tasnia ya fialmu, taasisi hiyo imekuwa ikiyumba na kwa kiasi kikubwa imeonekana kushuka kwa hadhi yake na hata wanachama wengine kuonekana kukatataa.
 
Alisema tangu alipochaguliwa mwaka jana, katika kikao ambacho kilimpa madaraka ya kuingoza Bongo Movie, mwenye kiti huyo hakuwahi kuitisha  kikao chochote kwaajili ya kujadili suala lolote na wanachama wake.
Aidha alisema pia kulikuwa na matamasha mbalimbali yaliyotokea kipindi cha uongozi wake, lakini hadi leo hawajui fedha zilizopatikana zimeishaje, kwakuwa taasisi hiyo haina akaunti ya benki, labda wamesema ingekuwa imewekwa huko.

Mafufu alisema hata baada ya kufika mwisho wa uongozi wake wasanii hao, aliwapigia simu kwa kuwataarifu kwamba uongozi wao umefika mwisho na kuwataka kujumuika pamoja ili kuweza kupanga ni jinsi gani ya kuitisha uchaguzi mpya.
 
Alisema uongozi huo baada ya kupata taarifa juu ya kuwepo kwa kikao cha kuanza kwa mchakato wa uongozi mpya, lakini hakuna hata msanii mmoja kati ya uongozi ule uliopita aliyekuja.
 

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi