Monday, December 23, 2013

Gomesa Tv

Makala: DNA (Kizazi) filamu ikajichanganya na maisha ya kweli@ Tito na mkewe Pamela     Kuvunjika kwa makundi mengi ya muziki, na maigizo hupelekea baadhi ya malengo waliyopanga kuvunjika na kuwa kama ndoto.
Mkundi mbalimbali ya sanaa yalianzishwa na  kujipatia umaarufu mkubwa,  kama ilivyokuwa kwa Fukoto, Kaole na mengine.

Hata hivyo  mwisho wake ni mpasuko mkubwa na hata kufa kabisa kwa makundi hayo, na kushindwa  kabisa kurudi na kufikia malengo waliyopanga mwanzo.
Lakini  tofauti sana kwa waigizaji Mrisho  Zimbwa maarufu kama Tito Carlos na mwigizaji mwenzake Pamela Brown ambaye sasa ni mkewe anayejulikana kwa jina la Shadya Brown.

Walipoamua kuungana kwaajili ya kufanya kazi pamoja ya filamu, na kujikuta katika vituko na mikasa iliyopelekea hata kutaka kutoka roho ya mmoja wapo, na hatmaye wanatimiza malengo  kwa kukamilisha filamu hiyo ingawa kulikuwa na kusuasua kwa muda mrefu.

Kukamilika kwa filamu ya Kizazi ambayo mbayo mwanzo ilikuwa ikijulikana kama DNA, na nilipoona baadhi ya scene na kugundua ni filamu nzuri na yenye kuvutia, kulinifanya nifanye mahojiano Tito ambaye ndiye mwenye filamu.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii, Tito alisema tayari ameshaikamilisha filamu hiyo,  ambayo inamuda wa zaidi ya miaka  mitatu na miezi.
Alisema kukamilika kwa filamu hiyo ni baada ya misuguano ya muda mrefu na  kuamua kuyaweka matatizo yao pembeni.
“Tumepitia misukosuko mingi ya maisha, lakini  tumeamua kuikamilisha na sasa inatarajia kuingia sokoni muda si mrefu,” anasema.
Miongoni mwa misukosuko ambayo ilitokea wakati wakiifanya  filamu bado haijakamlika.
Tito akiwa na Bibi Hindu kwenye filamu ya Kizazi

Kipindi filamu hiyo inaanzwa kuigiza, Pamela alikuwa bize sana na kazi, hivyo akawa sehemu ya uongozi wa filamu na sio mwigizaji.
Hata hivyo baada ya filamu hiyo kuanza miezi kadhaa, ndipo patashika likaibuka baada ya mwanamke kutokuwa na imani na mwigizaji wa kike aliyeigiza na mumewe.
Maelewano yakawa hamna ukizingatia yeye pia ni kiongozi, maafikiano yaliyoamuliwa ni kuondoa sehemu zote ‘Scene’ alizoigiza yule mwigizaji wa kike,  ikawa sababu ya Pamela kuamua kuingia mwenyewe na kushika nafasi hiyo.

Ingawa alishika mwenyewe nafasi zote alizotaka kuigiza yule mwigizaji wa kike, vikaja kuchanganyika na kazi ndipo akajikuta akikosa muda wa kuigiza na kupelekea filamu kuendelea kubaki kimya.
Likaja tukio lingine kubwa kiasi cha nusura kutoa roho ya mmoja wa wapenzi hao, pale mwaka 2011 baada ya Tito kupata ajali mbaya.
Tito anasema baada ya matatizo ya muda mrefu na mpenzi wake kabla ya kuwa mkewe, kipindi hicho akiwa mjamzito.

Ulitokea ugonvi mkubwa, ambao alishindwa kuvumilia ndipo alipoamua kuondoka nyumbani  Magomeni, na kuelekea Bilicanas kwaajili ya kupunguza mawazo.
Akiwa katika klabu hiyo ya usiku pamoja na Ben Branco, anasema akili zake zilikuwa zikimchanganya zaidi  akaamua kujituliza kwa kunywa pombe.
Anasema ilipofika muda wa saa saba, ndipo walipoamua kubadili klabu na kutaka kwenda Maisha Club.
 
Tito akiwa na mkewe Pamela
Ilibidi kutumia usafiri wa Pikipiki ambayo mara nyingi alikuwa akiutumia, ingawa wenzake walimkataza lakini hakuweza kusikiliza hata kidogo.
Ilibidi kufuatana na wenzake waliokuwa ndani ya gari, na yeye akiwafuata nyuma kwa pikipiki.
Hapo ukichanganya pombe, na mawazo mazito alipofika  daraja la  Salender, akajikuta akiwaza zaidi juu ya mpenzi wake na hata kupelekea kushindwa kulidhibiti pikpiki na kujikuta akipata ajali kubwa.

“Kosa kofia ya pikipiki ilibidi nipasuke kichwa, lakini nilinusurika”
Katika ajali hiyo, aliweza kuchubuka vibaya sana na hata kulazwa na baadaye kutolewa huku akiwa bado anamatatizo ya kichwa.
Hapo ndipo familia ilipokuja juu na kutaka aachane na huyo mwanamke, na mpango wa filamu yao ya DNA ukawa umeishia hapo.

Ilichukua miezi kadhaa kati ya Tito na Pamela kila mmoja akiamini hatoweza kurudiana na mwenzake, lakini kila mmoja alijikuta wa wakati wake akijiraumu na kuungana tena.
Kuungana kwa mapenzi yao suala la kuiendeleza filamu ya DNA lilirudi tena na kuwa na imani, ipo siku litaisha.

Katika tukio lingine ambalo hawatakuja kulisahau baada ya kujifungua mtoto wao, ambaye pia ni wa kwanza kwao anayeitwa Natalia.
“Lilikuwa tatatizo jipya ndani ya familia, lakini likawa kubwa sana kiasi cha kufikishana mahakamani” anasema.
Wivu wa mapenzi ulizidi kutawala, kiasi cha kipigo kuwa sehemu ya maisha yao na hata kutokuwa na maelewano hadi kufikishana mahakamani.

Mwaka 2012 baada ya kufungua kesi na ndipo mambo yalipovunjika tena, na kusitisha filamu ya DNA na ndipo Tito aliamua kutaka kutoa Scene zote zlizomweka mkewe na kumweka mtu mwingine.
Lakini ukubwa wa ghalama ulimfanya asubiri, huku akiudhulia mahakamani baada ya kufikishwa na mkewe.
Hata hivyo wakati kesi yao ikiendelea mlalamikaji akiwa Pamela na familia yake, juu ya Tito mambo yalikuwa tofauti kwa wao.

Kesi iliendelea na wakati huo wakijisurisha wenyewe nyumbani, hadi mwisho wa siku wakawa wanatoka katika chumba kimoja kwenda kwenye kesi, jambo ambalo liliangusha mshangao mkubwa kwa watu wanaowajua.
Kweli mapenzi ya watu usiyaingilie, leo hii Tito anasema tayari wameshamaliza migogoro yao yote na wameshakamilisha filamu ya DNA, ambayo wameamua kuipa jina la KIZAZI.

“Filamu muda wowote inaweza kuingia sokoni, na tumeona haina haja ya kuendelea kurumbana na kupoteza fedha nyingi”
Tito jina lake harisi ni Mrisho Salehe Zimbwe akiwa ni mtoto wa 5, mzaliwa wa Tanga pia ni baba wa watoto watatu, Amina, Abdulimajid na Natalia.
Baada ya kuingia jijini Dar es salaam, akajiunga na kundi la sanaa la Kaole, mwaka 2002  na kuwa miongoni mwa wasanii wa mwanzo wa kundi hilo.
Filamu yake ya kwanza kuigiza ni Chumba no 77 ambazo zilikuwa filamu za mwanzo, na kuleta mapinduzi makubwa hadi sasa.

Filamu ambazo amekuwa akifanya vizuri sana ni zile za mapambano, kwakuwa watu aliokuwa akifuata nyayo zao ni Jimmy Master na Kaini.
Mwisho

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi