Wednesday, December 18, 2013

Gomesa Tv

Makala; Batuli na ndoto zake Baada ya kuangaika kwa muda mrefu katika tasnia ya filamu kwa kucheza filamu za watu, mwigizaji Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ameamua kueleza juu ya mikakati yake mpya katika filamu baada ya kupata meneja wa kumwezesha katika kazi hizo.

Akizungumzia ndoto zake nyota huyo, ambaye alishawahi kufanya kazi nzuri katika filamu ya Fungate, Glory of Ramadhani, Waves of Sorrow huku akishirikiana na wasanii Kama Steve Mangele ‘Steve Nyerere’ Vicent Kigosi ‘Ray’, marehemu Steven Kanumba, Issa Mussa ‘Cloud 112’ na wasanii wengine kibao ambao ameshafanya nao kazi.

Batuli anasema kwa muda mrefu alikuwa akitumikia filamu za watu, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutambuliwa na kujilikana zaidi.
Lakini anasema kikubwa alikuwa bado alikuwa hajakamilika katika kufanya kazi zake mwenyewe hususani katika upande wa bajeti, kwakuwa hakutaka kufanya kazi zilizopoa na kudorola.

Kwa sasa nyota huyo ambaye anaumaarufu mkubwa, anasema amejipanga kuachia filamu zake tatu tofauti, ambazo pia  ni filamu zake za mwanzo chini ya uongozi wake mpya.
Anasema tangu alipoingia mkataba na meneja huyo mpya, zaidi ya miezi miwili iliyopita hivi sasa tayari ameshaanza kuandaa filamu tatu mfuririzo pamoja na matangazo ya Tv.

Batuli anasema filamu yake ya kwanza inaitwa Wekeza Inalipa, ambayo pia ameifanyia kipindi katika moja ya stesheni za Tv ili kuhamasisha watu kuwekeza hasa katika hisa.
“Katika filamu hiyo huwa nazungumzia umuhimu wa watu wa kununua hisa, ni moja ya filamu zangu za tofauti sana na nzuri kwa mimi naikubali sana,” anasema.

Filamu hiyo anasema imeambatana na matukio ya mbalimbali ya kutoa elimu na  kuwafunza watu waweze kujali zaidi maisha ya baadaye, hasa kwa kununua hisa ambazo zinaweza kusaidia maisha yao kwa kupambana na umaskini.
Zaidi ya filamu anasema pia amefanya kipindi  akiwa kama mtangazaji, katika moja ya stesheni ambazo zitakuwa zikionyesha tangazo hilo la Wekeza Inalipa.
Filamu yake ya pili anasema kwa sasa ndiyo ipo kwenye mikakati ya mwisho katika uchanganyaji wa picha ‘Editing’, ambao ameshirikiana na wasanii kutoka Afrika mashariki na kati.

“Kwa sasa bado sijaruhusiwa kuwataja wala kutaja jina la filamu kwakuwa bado tupo kwenye mkakati wa kuahkikisha inaisha na kuitangaza kabla ya kuingia sokoni” anasema.
Anasema kazi hizo zote zinampa moyo juu ya matarajio yake ya kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa wa Afrika mashariki na kati na Afrika nzima, katika suala zima la filamu.

“Tunaelekea vizuri katika kazi nzuri ya filamu, ambao itawezesha wasanii kufika mbali hususani kutokana na malengo yetu” anaendelea kusema.
Batuli anasema hivyo amejipanga amejipanga zaidi kufanya filamu zenye stori nzuri na zenye mvuto, kuanzia mavazi hadi waigizaji ili kupamba na soko la kimataifa kuliko kuangalia zaidi soko la ndani.

Kuhusu kuwa na meneja anasema maamuzi yake ya kutafuta meneja kwaajili ya kazi yake, si kwamba alikurupuka kuwa na  meneja ilimradi meneja.
Isipokuwa alifikiria na kuamua kutafuta meneja ambaye anawez kusimamia kazi yake, na kumfikisha katika kiwango cha kimataifa zaidi.
Anasema wasanii wengi wamekuwa wakiangaika wenyewe bila ya kuwa na uongozi, au meneja atakayeweza kusimamia vizuri kazi zake, kwa tena kwa sheria za nchi.

“Anasema wasanii wengi wamekuwa hawana elimu  ya kutosha,  kuhusiana na usimamizi wa kazi zao, na ndio maana wamekuwa wakiburutwa bila ya kujua washike wapi” anasema.
Hivyo kwa msanii kuwa na meneja kutamsaidi  baadhi ya kazi zake za sanaa kuwa chini ya usimamizi mzuri, bila ya msanii  kuathirika na chochote.
Anasema mara nyingi wasanii wengine wanatafuta mameneja ambaye, hawezi kumsaidia isipokuwa meneja ndiyo anamtegemea msanii.

Batuli anasema meneja ni lazima  aijue biashara ambayo anaenda kuiwekeza,  na kujua hasara na faida ya kazi yake.
Kufanya hivyo kutamwezesha kuweza kufika mbali, kwa msanii na meneja mwenyewe.

“Kama ninakuwa na  wazo la simulizi ya filamu, huwa nalifikisha kwa meneja wangu, ambaye naye anakuwa na watu wake kwa pamoja wanaiangalia na kuniambia na baadaye kufanya kazi baada ya kuona inafaa” anafafanua zaidi.
Anasema hiyo ndiyo kazi kubwa ya meneja wake na kama kuna lingine basi huwa wanakaa chini na kujadiliana, ili kufika mwafaka.
Kwa sasa Batuli anasema lengo lake ni kufika katika anga za  filamu za kimataifa za zenye kiwango cha juu, ikiwemo kuwashirikisha waigizaji   kutoka na wenye uwezo mkubwa wa kuigiza.

Kwa muda wa miezi miwili, anasema tangu  aingie mkataba na meneja huyo, anasema tayari ameshaanza kuona mafanikio makubwa ambayo anaamini, yatamwezesha kufika mbali zaidi.

Nyota huyo pia amesema hapendizwi na wasanii wanaovaa nguo za fupi na zenye kuonesha sehemu ya mauongo yao.
Anasema kuvaa za namna hiyo,  sio kwamba wanaweza kusaidi kazi zao kuuzika, ila wanajidhalilisha kutokana na Watanzania sasa wamebadilika na wanaangalia kazi zaidi.

Anaendelea kusema kwamba ingawa ni  maarufu, lakini hajalewa na sifa na ndiyo maana ameamua kujikita zaidi katika filamu za kiwango cha juu.
“Siku hizi watu hawaangali unavaaje? au mzuri kwa kiasi gani isipokuwa wanaangalia kazi yako ipo vipi” anasema.
Batuli anasema kwa sasa nguvu zake zote amaeamua kuwekeza kwenye kazi zake mpya, ili kuweza kufanikiwa na kujenga jina kubwa.
Batuli anasema yeye ni mama wa mtoto mmoja, alianza kuigiza mwaka 2008 katika filamu ya Mkasa.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi