Thursday, December 5, 2013

Gomesa Tv

Afande Sele afunguka juu ya Chadema

 
 Mkongwe katika Muziki wa Bongo Fleva, Seleman Msindi amefunguka kwa mara ya kwanza tangu alipochukua kadi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo 'Chadema' na tatizo ambalo linawakuta Chadema kwa sasa.
Afande Sele anasema hivi sasa yeye ni mwanachama halali wa Chama hicho, ingawa muda mrefu alikuwa akishabikia na wala hakusema yupo chama gani.
Kuhusiana na lengo lake na kutaka kugombea Ubunge Morogoro mjini, Afande alisema hilo sio lengo lake ingawa kama atapewa nafasi hiyo anaweza kuitumia vizuri.
Anasema sababu ya kujiunga na Chama hicho, ni kutaka kupambana kama mwanachama wa kawaida, na suala la Uongozi linategemea chama chake, kama kitaamua kumpa malaka ya kuweza kuongoza na sio yeye kujipangia kwakuwa yeye anategemea chama.
Alisema kwa muda mrefu alikuwa akiongea na wananchi kupitia muziki na kujaribu kuwafikishia wahusika, ujumbe wa kitu gani wananchi wanahitaji lakini anasema ujumbe wake huo umepuunzwa na ndiyo maana ameamua kuingia mwenyewe kwenye siasa.
Anasema kwa haya machafuko yanayotokea kwa sasa ni sehemu ya mapinduzi ya kila siku ya kichama na hayawezi kuwaathiri chama hicho zaidi ya kuimarika.


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi