Wednesday, December 11, 2013

Gomesa Tv

12 Desemba B'day ya Izzo@ Kuzindua wimbo mpya

 
MSANII  nyota wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Simwinga ‘Izzo B’ amesema ni kawaida yake kuachia wimbo mpya siku ya kuzaliwa kwake Desemba 12, lakini mwaka huu hajajua atatoa kwa mtindo gani.

nyota huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo Love Me akiwa na Elias ‘Barnaba’ na Sarah Kais Shaa, alisema kwamba ni kawaida kutoa wimbo kila inapofika tarehe hiyo, isipokuwa uzinduzi wa wimbo ndio unatofautiana.

tayari ameshakamilisha nyimbo nane, na kati ya hizo moja ndiyo inapaswa kutoka siku hiyo jambo ambalo anaamini peke yake hawezi kuchagua bila ya wadau wake.

“Nina nyimbo nyingi  nilizofanya ila nahitaji kukaa na watu wangu ambao wananishauri na kujua ni wimbo gani niutangulishe kuutoa” alisema.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi