Saturday, November 23, 2013

Gomesa Tv

Wakulima wa Korosho Mkuranga kulipwa fedha zao zilizopotea 2011-2012  NAIBU waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,  Mheshimiwa Adam Kighoma Malima, amewataka Watendaji na Viongozi wa Vyama vya ushiriki vya mkoa wa pwani, kulipa 2 .5 bilioni  kwa kusababisha harasa na upotevu wa fedha za wakulima wa Korosho.

Akitoa tamko hilo katika kijiji cha Kuruti, kata ya Chungubweni wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, alisema katika msimu wa 2011 na 2012 wakulima wa Korosho mkoa wa pwani, waliwasilisha madai ya kutolipwa fedha zitokanazo na biashara ya Korosho.

Alisema ndipo wakamtuma Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika, aliendesha ukaguzi wa hesabu za vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS)ambao ulithibitisha madai ya wakulima na kubaini hasara na upotevu wa fedha hizo.
 Aidha alithibitisha kwamba wahusika wakuu wa upotevu wa fedha za wakulima ni Wajumbe wa Bodi na Watendeji wa Vyma husika vya Ushirika.
Katika ukaguzi huo kiasi cha sh.3,057,794,500, kilibainika kupotea kwenye vyama vya Ushirika 97, na kiasi hicho kinahusisha deni la sh. 2,567,056300, la vyama 69 vya wilaya ya Mkuranga.


Mhe, Malima alisema kwa mujibu wa kifungu cha 93 (2) cha sheria ya vyama vya ushirika ya mwaka 2003, Mrajis wa Vyama Vya  Ushirika, aliandika Notisi za madai kwa kila Mjumbe wa Bodi na Mtendaji aliyebainika kushiriki, katika hasara na upotevu.
Na kuwaamuru kulipa fedha kulingana na hasara au upotevu uliojitokeza kwa kila AMCOS, ili kulipa fidia au hasara walizosababisha.
Katika notisi za Madai wahusika walielezwa haki ya kukata rufaa kwa Mhe. Waziri mwenye dhamana ya Maendeleo ya Ushirika, ndani ya siku 30, kuanzia  tarehe ya kupokea Notisi za Madai.
Alisema baadhi ya wahusika waliamua kukata rufaa kwa Mhe. Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika, wakidai kwamba wao hawakuhusika na hasara  iliyotokana na uzembe na ubadhirifu uliokea, hivyo kumuomba Mhe. Waziri wasilipe deni hilo.
Jumla ya rufaa mia nne therasini  nne(434) ziliwasilishwa kwa Mhe. Waziri, ili kutendea haki kwa wahusika, uchunguzi wa rufaa hizo ulifanyika kwa kuzingatia nyaraka zilizowasilishwa kwa Mhe. Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika.
Hivyo amekubaliana na maamuzi yaliyofanywa na Mrajis, Mhe. Waziri ameona kuwa hasara hizo zimetokana na uzembe na ubadhirifu wa wajumbe wa Bodi na Watendeji kwa kuidhinisha malipo yasiyo halali.
Hivyo Mhe. Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, amezikataa rufaa zote na kuwaagiza, kila Mjumbe wa Bodi na Mtendaji wa Chama cha Ushirika,  kilichohusika kulipa deni kwa mujibu wa Uchambuzi, uliofanywa na Mirajis ndani ya siku kumi na tano (15).
Kwa mujibu wa sheria ya Vyma Vya Ushirika, ya Mwaka 2003, Mirajis atamchukulia mra moja hatua za kisheria, za kumfikisha Mahakamani, hatua hizo za kisheria ni pamoja na kumfungulia kesi ya jinai kwa kosa la ubadhirifu.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi