Tuesday, November 26, 2013

Gomesa Tv

Saba wafa,21 majeruhi ajali Chang'amboe@Tanga

Watu saba wamekufa papo hapo na wengine 21 kujeruhiwa vibaya katika eneo la Chang’ombe, Barabara ya Segera – Chalinze, wilayani Korogwe, Tanga baada ya mabasi mawili madogo ya abiria waliyokuwa wakisafiri kugongana uso kwa uso.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alisema jana kwamba ajali hiyo ilitokea juzi saa 10:20 jioni baada ya gari moja kukwepa mbuzi waliokuwa wameingia barabarani.
Alisema majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Magunga.
Alisema kati ya waliofariki, watatu walitambulika majina yao akiwemo dereva wa moja ya mabasi hayo aliyefahamika kwa jina moja la Kombo. Wengine ni mkazi wa Muheza, Martin Simon (35) na mkazi wa Korogwe, Juma Abdallah (37).
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Valerian Richard (27), Mohamed Juma (60), Halima Abbas (35), Ali Rashid (61),  Asha Bakari (39), Rehema Hassan (39), Ibrahim Ramadhan (26), Omari Issa (30), Issa Ibrahim (30) na Shaaban Hamza(35)
Wengine ni Ramadhan Mdangula (30), Mwanahawa Selemani (25), Mariam Ramadhan (24), Theresia Gabriel (35), George Ernest (25), Issa Mohamed (32), Fatma Hassan (48), Sharifa Bano (40), Shida Bano (27), Abel Elia (35), Fadhil Rajabu (28) na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Marijani.
Kamanda Massawe alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na mwendo kasi wa mabasi yote mawili.
Akizungumzia matukio ya ajali na kuelekea mwisho wa mwaka, Kamanda Massawe aliwataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuacha kuendesha magari kwa kasi.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi