Kwa mara ya kwanza naweza kusema
kushinda kwa filamu zenye asili na mazingira ya Kiswahili kama Mdundiko, huenda
ikawa imewabadilisha kidogo Watanzania na kufanya filamu za Kitanzania na Kiafrika.
Unaweza
ukawa mwanzo wa kubadilika kutoka katika
filamu yenye mahadhi ya Kizungu na kuanza kutenengeneza filamu za kwetu
kwaajili ya kuutangaza utamaduni wetu katika nchi zingine.
Miongoni mwa
wasanii walioamua kubadilika ni Single Mtambalike, maarufu kama Rich Richie.
Akizungumza
na mwandishi wa makala hii, kwamba
tayari amesha kamilisha filamu yake ya Kitandawili, nikiwa kama mwandishi na mdau nikapata nafasi
ya kuiona na ndipo nikapata nguvu ya kuandika makala hii.
Single
mwenyewe anasema filamu hiyo aliamua kuifanya baada ya kugundua nchi
zilizoendelea hawahitaji tena kuona nyumba za thamani.
Wala magari
ya ghalama , kwakuwa nchini mwao ndipo wanamotengeneza vitu hivyo na kutuletea
sisi, tena wao wanavyo bora zaidi ya
vyetu.
Anasema
ndipo akatafuta mkoa mzuri wenye mazingira ya kutosha na kuamua kwenda kwaajili
ya kufanya filamu ya Kitandawili.
Anaelezea
kwa kusema kwamba ingawa filamu za kutoka nje ya mkoa huwa ni ghalama sana,
lakini hudumu kwa muda mrefu na hata ukiingiza kwenye tuzo za kimataifa uhakika
wa kushinda ni mkubwa.
Filamu anasema
wameifanya katika mkoa wa Kilimanjaro,
wilaya ya Same kijiji cha Ndungu, chenye
mazingira ya asili zaidi ambayo bado hayajaharibiwa sana.
(Haji Adam akiwa na mpiga picha Koba) |
“Tanzania
kuna sehemu nzuri za kuvutia ambazo tunaweza kuzitangaza kupitia filamu zetu.”
Anasema hata
hivyo ghalama kubwa sana zikaja juu ya kutafuta mazingira mazuri ya kuigiza,
ili mbidi aende Kilimanjaro kwa safari zaidi ya moja hadi alipofanikiwa kupata
kijiji hicho.
Baadaye
alirudi Dar es salaam na kubeba kundi la
watu 19, kwaajili ya kazi hiyo ingawa wengine ilibidi kuwakodisha huko huko,
ili kuwapa ujuzi zaidi.
“Watu huwa
wanakimbia gahala za kufanya nao kazi
kwa kubeba watu, kutoka nao Dar es
salaam.”Anasema.
Anasema
kundi la watu 19, kuwapangia hoteli na vyakula pia na usafiri wa kutoka Dar es salaam, kitu ambacho watu wengi
wamekuwa wakikikimbia.
Lakini baada
ya kufanikisha ghalama hiyo, ndipo utakapoona uzuri wa filamu hiyo ambayo
imepambwa na mazingira.
“Nashukuru
Mungu filamu tumepata mazingira mazuri, sana ambayo yaliendana na Hadithi
yenyewe.”
Labda na
mimi ningekudokezee baadhi ya vipande
katika filamu hiyo, na kukuambia kwanini nimesema muda umefika wa Tanzania kuchukua tuzo za
Kimataifa kwa filamu zetu.
Waigizaji wa
filamu hiyo, yupo Haji Adama ‘Baba Haji’,Irene Vede mwigizaji mpya ambaye
anafanya vizuri sana, Single Mtambalike ‘Rich’ Mr Kupa, Kinyambe, waalimu wa
Chuo cha Bagamoyo Mzee Maeda, na Ilenjwa Mtake.
Hao naweza
kusema ndiyo waliofanya vizuri zaidi, ingawa wapo wazee wengi kutoka mkoani
humo, pia wapo vijana wengi kutoka Dar es salaam na Kilimanjaro.
Filamu
inamwelezea kijana ‘Rich’ aliyekuwa akitafuta maisha kwenye dunia hii ya
tabu, hadi kufikia kwenye kambi ya
Wakimbizi huku Burundi.
Katika
tafuta zake za maisha anajikuta anazama kwenye penzi la Binti wa Kiburundi, na
kuamua kumchua kurudi naye kijijini kwake.
Lakini kubwa
linakuja pale anapoingia kijijini bila ya kuwa na mafanikio, zaidi ya kuongeza
mtu kwenye familia jambo ambalo linazua mzozo wa kifamilia kutoka kwa baba yake
mkorofi ‘Mzee Ilenjwa’.
Anaamua
kuanza safari nyingine ya kwenda kutafuta jijini Dar es salaam, na kumwacha
mkewe ndani ya familia ambayo tayari ilishaanza kumchukia.
Lakini stori
inakuja kushika moto, baada ya Rich kurudi kijijini akiwa na fedha kidogo za
kufungua genge, ambalo linaleta heshima kwenye familia yao.
Tatizo kubwa
ambalo utapenda kuliona, ni hali
aliyomkuta nayo mkewe baada ya kurudi kutoka Dar es salaam, na jinsi alivyoweza
kutaabika hadi kutegua kitandawili hicho, ambacho kina matukio yanayobeba
ukweli wa maisha ya kijijini na kukufanya mwili kusisimka.
Huo ni
miongoni mwa uhondo wa filamu hiyo, kwa mimi naweza kusema ni miongoni mwa
filamu abazo zinapaswa kutizamwa na Watanzania na nchi zingine kutokana na
kubeba utamaduni wetu.
Kama
hutovutiwa na mazingira mazuri ya mawe makubwa yaliyojipanga mtoni, basi kipo
kingine cha kukuvutiwa kama Ziwa kubwa na mitumbi ya wafanya biashara wa samaki.
Ni tofauti
na filamu zingine, humu utapenda kuona wazee wapya anavyoweza kuigiza na kutupa
taswira na kutukumbusha wazee wa kijijini wanavyopenda kuamrisha, na hata
kuchukua sheria mkononi.
Pia utapenda
kuona kijiji kizuri wakati kikimwilikwa na jua la alfajiri huku ukungu ukifanya
anga lipendeze, hali ambayo tumezoea kuona kwenye filamu za nje.
Naweza
kusema hongera Rich, kwamaana unaanza kuitangaza Tanzania kutokana na filamu
hii ya Kitandawili.
Lakini kubwa
ninalolikumbuka alilosema Rich kwamba,
“Filamu za
kuonyesha magari na majumba ya kifahari, sasa basi.”
Nami
namuunga mkono, na kuwaambia waigizaji
wengine wa Tanzania, kabla ya kuisifia filamu yako ina gari la ghalama
kama Hammer, jiulize lengo la kazi zako
ziende wapi? Kama zibaki Tanzania sawa, kama zienda Kimataifa elewa huko ndipo
walipotengeneza hilo Hammer.
Mwisho
https://www.facebook.com/gomesamohamedi