Saturday, November 23, 2013

Gomesa Tv

MAKALA; Irene Poul alifunguliwa mlango na Kanumba@ Yeye akafunga mlango wa KanumbaHUENDA usishaagae kuona wasanii wengi wa filamu kuona wakimiliki magari ya thamani, huku ukijiuliza kwa filamu gani walizocheza mpaka kumiliki magari hayo.
Lakini kikubwa unaweza kujiuliza kwanini wasanii wanaomiliki magari hayo ni wanawake na wanaume wamekuwa wakiangaika, na kulalamika kwamba maisha ni magumu.

Lakini kwa msanii mwenye mvuto wa aina yake na kipaji cha kipekee, Irene Poul, yeye amekuwa tofauti sana, kuhusiana na maslahi makubwa ya wasanii wenzake kwa kazi ndogo wanazofanya.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii, Irene anaelezea zaidi kwa jinsi wasanii wengi wa kike wanavyojikuta wakishindwa kuendesha kampuni zao za filamu kutokana na vikwazo wanavyokutana navyo.

Anasema alipoingia kwenye tasnia hiyo, aliamua kufanya iwe  kazi hivyo alijikuta akifanya kazi nyingi bule kwakuwa alikuwa akitafu ta jina na umaarufu.
“Nilikuwa najua nini nakifanya, hivyo nikawa nafanya kazi nyingi za watu bule bila ya malipo” anaelezea.

Kwakuwa alikuwa akiigiza filamu za watu anasema alianza kutumikishwa, kama kulazimisha kumkisi mtu na hata kuonyesha vitu vya kimapenzi, ingawa kwake alikuwa akiona zipo njia nyingine kwa kuonyesha hisia za wapenzi bila kupeana kisi.
Vitendo hivyo anasema vilianza kumfanya kutamani kuigiza filamu zake, ambazo atatumia hisia za kimapenzi zaidi kuliko vitendo.
Anasema kwakuwa alikuwa hana uwezo, hivyo ilimlazimu kuendelea kutumikishwa.

Lakini anasema hapo ndipo wasanii wengi, wanajikuta wakikata tamaa na hata kutumishwa biashara zingine kwa kuwa wameingia kwenye tasnia wakiwa na malengo mengine.
“Ujue wasichana wengi wanaoingia kwenye tasnia ya filamu, wanakuwa hawajitambui na ndiyo maana wamekuwa wakishindwa kuendelea,” Anasisitiza.

Irene anasema mara nyingi , alijikuta akifikiria zaidi maisha yake ya baadaye hasa kwa wale wanaojifunza kupitia yeye.
Anasema pia alikuwa akijiuliza ni jinsi gani baadaye atakuja kumwangalia mwanaye, kama akifanya vitu ambavyo baadaye vitamsuta katika jamii, kwa kuigiza filamu za kuvaa ovyo, au kwenye biashara iliyonje ya sanaa.

“Niliweza kukua kisanii ingawa  kipato ambacho nlikuwa nikipata kilikuwa hakikidhi mahitajii,” anaelezea zaidi.
Irene anasema lakini baada ya kuhangaika kufanya kazi za watu ndipo alipojipanga kufanya kazi zake mwenyewe.
Hapo ndipo akajipanga na kufanya filamu yake ya kwanza aliyoipa jina la  Kalunde.
Anasema kufanya filamu hiyo kulimsumbua sana kutokana na uchanga wa kufanya filamu zake.
Changamoto alizozipata zilimchosha kiasi cha kufanya kitu kwa ubora ambao hakutarajia.

Anasema Lengo lilikuwa kutoa filamu ambayo ilikuwa na kiwango cha juu, lakini alijikuta akishindwa kukamilisha lengo hasa kutokana na  bajeti.
Kutokana na ufinyu wa bajeti, anasema  kazi nyingi kama  kuwaendesha wasanii,  kutafuta maeneo ya kuigizia ‘Location’, Production Mananger  zote alikuwa akizifanya mwenyewe.
 “Hapo ndipo nilipogundua ugumu wa kazi hii, lakini nikajitahidi hivyo hivyo na kazi ikaisha,” anaendelea kuelezea msanii huyo.
Anasema lakini kubwa zaidi likaja juu ya kampuni ambayo alilipa fedha, kwaajili ya kukamilisha  production, ili kupewa filamu yake.
Kwakuwa alikuwa mgeni katika masuala ya kuigiza, anasema hakujua kama makampuni ya ‘Production’ huwa hayalipwi fedha zote kutokana na usumbufu wao.

Kwakuwa alimlipa fedha zote, alijikuta akiingia kwenye usumbufu mkubwa kiasi cha kuchelewa kwa filamu yake.
“Ujue wanaume wanaweza kutumia nguvu, katika kukamilisha mambo yao na hata kumudu purukushani, ili kazi yao iende upesi,” anasema.

Filamu hiyo ilimsumbua kwakuwa wakongwe walimuona kama ni msanii mchanga, na kumchukulia ‘poa’, na kumdharau.
‘Kila mtu alikuwa akinichukulia poa kiasi cha kujikuta nafanya kazi nyingi kwa wakati mmoja jambo ambalo lilikuwa likinichosha sana” anasema.
Hata hivyo Irene anasema amekuwa msanii mwenye bahati sana, kwakuwa anajiamini.
Kwa mara ya kwanza kuingia kwenye tasnia, anasema ilikuwa  mwaka 2010 ambapo alicheza filamu  Morning Alarm.
Filamu hiyo pia zilikuwa miongoni mwa filamu  za mwanzo kabisa za marehemu Steven Kanumba akiwa chini ya mwongozaji ‘Director’ Gabriel ‘Mtiti Game’.

Akiwa katika filamu hiyo, aliweza kukutana na waigizaji wengine kama   Ben Branco na Patcho Mwamba.
“Niliweza kuwajibika vizuri kwa kuonyesha uwezo wangu kiasi cha kuanza kukubalika na watu wengi” anasema
Kuonyesha kwamba ni msanii wa kike ambaye amekuwa na bahati kubwa, yeye ndiye msanii wa mwisho kuigiza na marehemu Steven Kanumba, na Hussein Mkiet ‘Sharomilionea’ katika filamu ya Love and Power.

Irene anasema msanii ambaye amekuwa akimfuata nyayo zake kama kioo chake ‘Realy Model’ ni mwigiza wa Hollywood, ni Angeline Jolie.
Anasema zaidi ya kumpenda, lakini pia amefanana naye.
Filamu ambazo alizowahi kuigiza ni nyingi sana lakini zikiwemo,  Penzi la Kiza akiwa na Issa Mussa ‘Cloud 112’ na   Dereva Bajaji akiwa na  Salum Haji ‘Mboto’ ikiwa filamu ya vichekesho maarufu kama mtindo wa  ‘Romantic Comedy’.

Kwa sasa anasema anatarajia kutoa filamu yake ya pili ambayo itaitwa, Mjuto, akishirikiana na Slim Omari, Mama Wele, na Salma Jabu ‘Nisha’.
 “Hiyo ni filamu ambayo naandaa mwenye chini kampuni yangu, ambayo itakuwa nafanya kazi zangu mwenyewe.” Anasema nyota huyo. Mafanikio makubwa anasema aliyoyapata ni kuweza kumudu kuendesha kampuni yake ya Krema Production, kuwa na usafiri wake na kuweza kumudu maisha yake kwa kutegemea zaidi kazi ya filamu.
Mwisho

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi