Saturday, November 23, 2013

Gomesa Tv

MAKALA; Hivi unamjua vizuri Slim Omary?
  Kwa sasa jina la Slim Omari, limeendelea kung’ara katika filamu za Bongo, na kuwa miongoni mwa vijana wanaokuja kwa kasi na kushika filamu nyingi sana.  Nyota huyo si katika filamu pekee ambayo anafanya vizuri,  lakini tayari ameshaanza kushika soko la matangazo akiwa kama mwanamitindo ‘Model’ wa matangazo kwa kanda ya  Afrika Mashariki.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya vizuri na kupata mashabiki wengi ni, Kivuli akiwa na Wastara Juma, Waves of Sorrow ya Ray, Family War, I am Lost na nyinginezo.
Ndipo mwandishi wa makala hii, alipoamua  kumtafuta ili kuweza kujua siri ya kuvuma kwake na mafanikio ya muda mfupi, huku wengine wakimwona kama msanii mchanga.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii, anasema ni kweli katika tasnia ya uigizaji ni mchanga, kwakuwa alianga kuigiza filamu yake ya kwanza mwaka2011 ambayo iliitwa My Angel.
Anasema katika filamu hiyo, alikuwa na Yusufu Mlela, na Hemed Seleman, na hapo ndipo alipoamua kuanza kujikita zaidi katika tasnia hiyo.

“Mimi ni mchanga katika tasnia, ingawa kabla ya hapo watu walikuwa wakinishauri niingie kwenye tasnia hiyo nami nikawa nakataa” anaelezea.
Anasema lakini katika tasnia ya filamu na muziki wa Bongo Fleva, yeye si mgeni sana kwakuwa tayari alikuwa huko kwa muda mrefu sana.
Kipindi hicho anasema alikuwa nyuma ya kamera, ambapo alikuwa akifanya kazi tofauti na ambayo anafanya sasa baada ya kuja mbele ya kamera ambapo watu ndipo wanamuona.

Slim anasema   kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza mafunzo yake, akiwa Afrika Kusini katika shughuli zake za kikazi, mwaka 2000 aliamua kusomea masomo ya muda mfupi kuhusiana na mambo ya Video  production.
“Nilikuwa tayari nashulikia masuala ya production, hivyo nikaona ni bora nisomee ili kuweza kuongeza ujuzi zaidi’ anasema.
Baada ya kurudi nchini alipata kazi kwenye kampuni moja lakini hakukaa nayo sana na baada ya hapo akaanza kufanya kazi kwenye kampuni mbalimbali za Production.

Kwa kipindi hicho anasema alikuwa akijihusisha zaidi, na upigaji picha wa video, za matangazo, muziki wa kizazi kipya na filamu kwa muda mchache.
“Nilikuwa nikijihusisha zaidi na kampuni za kutengeneza filamu, na muziki, matangazo na hata matamasha au mikutano ya viongozi mbalimbali,” anaelezea na kusema kwamba  aliweza kutengenza video za wasanii mbalimbali, akiwa na kampuni ya Visual Rab chini ya Adam Juma.

Anasema kwa kipindi hicho, pia alikuwa akifanya kazi kama mwongozaji wa filamu, ambapo alikuwa akisaidiana na Adam Kuambiana na Benjamini Busungi katika miongoni mwa kazi zake za filamu.
“Niliweza kupata uzoefu kwakuwa nilikuwa nafanya kazi nyingi na watu na watu wenye uzoefu, kiasi cha kuweza kujifunza vitu vingi zaidi anasema.
Baada ya kupata uzoefu ndipo alipojikita zaidi katika kuhariri picha za video za muziki, na filamu.

Kwakuwa  alikuwa akifanya kazi nyingi,  kwa kipindi hicho akiwa chini ya makampuni ya watu, ndipo alipoamua kufanya kitu kingine tofauti.
Anasema aliamua kuanzisha tamasha la Bongo Poem, kwaajili ya kusaidia vijana ambao walikosa nafasi ya kuingia studio huku wakiwa na uwezo mkubwa wa kuimba.

“Wakati nafanya kazi katika makamkpuni ya watu, watu wengi walinijia na kusema wanaweza kuimba hivyo wakahitaji zaidi mchangao wangu.”
Kutoka na hali hiyo ndipo akaamua kuanzisha tamasha hilo, ambalo lengo lake lilikuwa kuzunguka baadhi ya mikoa ya Tanzania, ili kupata vipaji vipya vya muziki na kuvisaidia.

Anasema wakati akiwa katika matamasha hayo, ambayo alianza nayo Dar es salaam, na mikoa ya jilani ndipo akapata tenda ya kufanya moja ya video ya vikao vya siasa kilichofanyika Msasani.
Wakati akiwahi kufunga mitambo ‘Project’ kwa ajili ya kuweza kupata matukio, ndipo njiani akakutana na foleni kubwa.
Kutokana na foleni hiyo, ndipo akaamua kushuka kwenye gari lake na kutafuta pikipiki ili kuweza kuwahi.
Lakini jambo ambalo anasema bila ya kutegemea ndipo akapata ajali mbaya,2009  maeneo ya darajani Mbezi kwa Komba na kumsababishia kuvunjika mguu, ambapo alikimbizwa hospitali kuwekewa vyuma kwenye mguu wake.

Slim anasema akiwa nyumbani na vyuma vyake mguuni, ndipo vijana wengi waliokuja kumtembelea wakamshauri kwamba ajiingine kwenye filamu kwakuwa hatoweza tena kuzunguka na kamera.
Anasema jambo hilo alianza kulifikiria mara mbilimbili, na kwakuwa alikuwa kitandani kwa muda mrefu ndipo wazo lakujikita kwenye filamu likaja.
“Nilikuwa najiuliza kwamba nitaweza kusimama kwa muda mrefu na kamera wakati vyuma vipo mguuni? Hapo ndipo nikaona ni bora nijikite kwenye kuigiza,” anasema.
Kwakuwa tayari alishafanya kazi na wasanii wakubwa, na alikuwa akiongoza baadhi ya filamu kama vile mchukuaji picha ‘Video Camera’ anasema alikuwa na upeo ingawa si mkubwa sana.

Baada ya kuanza kupona ndipo alipoamua kujikita kwenye filamu akianza na kuigiza filamu ya My Angel, ambapo alikutana na wakongwe kama Mlela na Hemedi.
“Baada ya kufanya vizuri kwenye filamu hiyo, ndipo sasa nikajikubali kwamba naweza kukaa hapo na kuendelea kufanya vizuri zaidi” anasema.
Anasema kadri ya kazi zake zilivyokuwa zikitoka ndipo alipozidi kupata mwaliko wa kafanya kzi nyingine zaidi kutoka kwenye makampuni za watu.
“Nilianza kupata kazi za kuigiza nyingi, mpaka nikawa nachagua zingine
Kwakuwa nisingeweza kuzifanya zote” anasema.
Baada ya hapo sasa akaanza kujikita katika kutengeneza matangazo ya bidhaa mbalimbali, ikiwemo Bel lager kwa Kenya na Uganda na hapa Tanzania alifanya zaidi ya Kumi.

Anasema pia amekuwa akifanya matangazo mbalimbali, kama ya Voda com, Tigo, Tulizana, na matangazo ya kampuni ya soko la hisa la Dar Es Salaam.
Anasema kwa sasa ameteuliwa kuwa balozi wa benki moja , ambayo kwa sasa inaitwa Commercial Bank, pia ni balozi wa nguo za kimarekani ambazo zinazuia kuharibika kwa ngozi kwa wageni, ambao wamekuwa wakisumbuliwa na jua.
“Baada ya kufanya mitindo wa mavazi yanayotengenezwa na Wamarekani, kwaajili ya kujilinda na jua ndipo wakaamua kunipa na ubalozi” anaelezea.
Kwa sasa malengo yake anasema kumalizia filamu yake ya Coast To Coast ambayo itakuwa filamu ya kwanza kutengenezwa mwaka nzima, na kuchukua wasanii  wa nchi mbalimbali.

Anasema filamu hiyo tayari imekutanisha wakari kutoka ujerumani, kama Van, Clara na Maria, Tanzania ni Batuli, Wastara Juma, Adam Kuambuana, Ben, Jamse, Tito, Muogo Mchungu, yeye mwenye na Mkenye mmoja.
Huyo ndio Slim Omari, ambaye ni  mzaliwa wa Dar es salaam,  baba yake mzee Omari alikuwa mtu wa Yemen lakini mama yake ni mswahili.
Shule ya msingi aesomea Temeke Magede, na kujiunga na Elimu ya sekondari ya Saba Saba International, na baada ya hapo akaendelea na kujiendeleza na masomo mengine.
Mwisho.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi