Friday, November 29, 2013

Gomesa Tv

Jengo la uwanja wa kombe la Dunia Brazil laanguka@ Watu 2 wafa papo hapo

 
 
Watu wawili wamepoteza maisha baada ya kubomoka kwa sehemu ya uwanja mpya wa mpira wa miguu unaojengwa kwenye mji wa Sao Paulo, uwanja mbao ndio unatarajiwa kutumika katika sherehe za kufungua mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Katika tukio hilo watu Wawili walimepoteza maisha, walikua miongoni mwa Wafanyakazi wanaojenga uwanja huo ambapo kubomoka kwa uwanja huu kulitokana na kufeli kwa crane ya chuma iliyokuwa ikitumika kuezekea paa la uwanja huo,ambapo waliofariki ni Fabio Luiz Pereira, 42, driver/operator wa crane ya kampuni ya BHM Munck pamoja na mjenzi Ronaldo Oliveira dos Santos, 44.
 
Brazil inajaribu kuhakikisha Viwanja vyote 12 vitakavyotumika kwenye mechi za kombe la dunia vinakamilika na ndio maana vimekua vikijengwa kwa kasi ilikuhakikisha vinamalizika kwa muda uliopangwa na FIFA ambao ni December 2013.
 
Hapa likiwa chini.

 
Lengo walitaka kuliona likiwa hivi baada ya kukamilika.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi