Wednesday, November 27, 2013

Gomesa Tv

Jadan na Will Smith si wa kwanza kuigiza baba na mwana@ Wengine hawa

Mnaweza wote kuwa waigizaji kati ya Baba na Mwana, lakini filamu ambzo mkaigiza wote pamoja zikawa chache au zisiwepo kabisa. Hawa ni miongoni mwa wasanii walioigiza filamu moja na watoto wao, Will Smith katika filamu  After Earth na mwanaye Jaden Smith ambaye tayari alishang’aa katika Karete Kid na Jack Chan.Robert  Downey Jr  ambaye aliigiza kama Irone Man 1,2,3 pia akaigiza katika filamu ya Avenger, naye aliigiza na baba yake anayeitwa Robert Downey Sr, ambaye ni mwandishi na Director ambaye maarufu kwa kutengeneza na kubana bajeti katika filamu zake katika miaka ya1960 na 1970. Ambapo waliigiza katika filamu ya Pound,  baba Sr  aliigiza kama kijana mwenye umri wa miaka 18, aliyekuwa akifuga mbwa na baadaye kumuokota mtoto ambaye ndiyo  Jr (Mwanaye).


James Caan  yeye alishawahi kuigiza na baba yake,  Scott Caan  mara mbili. Walicheza kwenye filamu ya 'A boy Called Hate mwaka 1995 na katika filamu Mercy mwaka 2009.

Ninapomzungumzia  Josh Brolin nadhani utamkumbuka zaidi katika filamu ya MIB (Men In Black) ambayo yupo Will Smith, nadhani umeshamkumbuka yule babu mwenye vituko.
Yeye na baba yake James, walikuwa kwenye filamu ya My Brother War, huku baba mtu akiigiza kama kiongozi wa mgogoro na mwanaye aliyeigiza kama ndugu yake akimsindikiza katika vita hivyo.


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi