Saturday, November 23, 2013

Gomesa Tv

Hizi ndo nzito za Zitto Kabwe@ What Next?Najua uwe mpenzi wa siasa, au si mpenzi wa Siasa, lakini kwa hili najua lazima utashituka kutokana na taarifa ya Chama cha Chadema juu ya kumvua  Nyadhifa zote,  Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama  kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.

Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu wamepewa siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama.
Lakini kikubwa bado watu wanajiuliza, nini kinafuata juu ya mwanaharakati huyu, aliyefanya vijana kupenda siasa? TUNANGOJE? Toa maoni yako kama unahisi unayo ya kutoa.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi