Fedha inaraha
yake bhana, nyota wa filamu na mwanamitindo kutoka pande za Marekani, Angelina
Jolie, amemnunulia mumewe Brand Pitt kisiwa kinachofanana na moyo.
Kisiwa ambacho
maili 50 kaskazini mwa Newyork Marekani,
amekinunua kwaajili ya kusherekea siku ya kuzaliwa kwa Pitt anayetimiza miaka 50.
Kisiwa hicho
wameamua kukiita jina la Petro, ambacho wamejenga nyumba kubwa za kifahari
mbili zikiwa zimebuniwa na Frank Lloyd
Wright, ambaye pia ni mshikaji wake Pitt.
Hii si mara ya
kwanza kwa mwanamama huyo, kwani mwaka 2011 siku ya kuzaliwa kwa Pitt, Jolie alimnunulia maporomoko ya maji yaliyopo California, ambapo Wright huyo huyo, aligewa
kazi ya kujenga bonge la mjengo juu ya maporomo hayo kwaajili ya makazi ya
wapenzi hao.
Mjengo unaotaka
kujengwa hapo, unatarajia kutumia zaidi ya dola za kimarekani 24 Milion.
Hadi sasa bado inasadikiwa wanandoa hao, ambao walicheza filamu ya Mr & Mrs Smith, mwanamke
anaongoza katika mauzo Duniani, na mwanamme anashika nafasi ya kwanza hadi ya
Tatu.
Jiulize wewe mwenzako, umemnunulia nini siku ya kuzaliwa kwake?
https://www.facebook.com/gomesamohamedi