Saturday, November 23, 2013

Gomesa Tv

Ben Poul kuinua vipaji vya Dodoma

Baada ya kufanya vizuri jijini Dar es salaam, msanii Ben Poul, amesema anataka kurudi nyumbani Dodoma kwaajili ya kukusanya wasanii wakali wa jiji hilo, ambao hawakupata bahati ya kufanya vizuri kwenye vyombo vya habari, ili kuwasaidia kuingia studio.


Ben Poul hivi karibuni pia aliwahi kwenda mkoani kwao huko, na kufanya matembezi na watoto i Katika Vituo Vya SHUKRANI ORPHAN CENTER (watoto yatima) & MIUJI CHESHIRE (Watoto wenye Matatizo ya Kiakili) vilivyopo mkoani Dodoma, ili kuonyesha mshikamaono na wakazi wa eneo hilo.
msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo kama JIKUBALI, amesema kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma, ataenda na wadau na wanamuziki, ambao wanaweza kuwasaidia wasanii wachanga wa mkoani humo.
Alisema wasanii waliofanya kazi lakini zimeshindwa kupata Air Time ya nguvu, basi atawasaidia kujulikana kupitia tamasha hilo, na wale wasiowahi kuingia studio, atahakikisha wanapata nafasi hiyo ya kujulikana zaidi.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi