Saturday, July 27, 2013

Gomesa Tv

Pendo Njau- Bingwa wa Kickboxer, aliyekimbizwa na ngono, adondokea Bongo Movie


Huenda ukawa hujui, lakini ndivyo ilivyo nyota wa ngumi Tanzania na Afrika Mashariki na kati Pendo Njau, ameamua kukimbilia katika uigizaji wa filamu baada ya kushindwa kuvumilia rushwa ya ngono iliyokuwa ikimwandama.
Hayo yalijitokeza baada ya kuhitajika kwenda katika pambano la K One, ambalo ni miongoni mwa mapambano makubwa yanayofanyika Japan, huku zikihusisha nchi tofauti za duniani.
Si nafasi ambayo kila mtu anaweza kuipata, lakini nguvu akili na ujasiri wa kushinda mapambano ya kimataifa ndiyo unafanya kutumiwa barua na uongozi wa ligi hiyo.
Hayo na mengine mengi, ndiyo yaliyomfanya mwandishi wa makala hii, kumtafuta na kutaka kujuzwa na kudadavuliwa zaidi.
Anajulikana zaidi kwa jina la  Pendo Njau lakini mwenyewe, anasema hilo jina lake lakini jina harisi alilobatizwa nalo ni Hellena Honest Njau, anasimulia na kusema matatizo yote yalianza baada ya pambano la mwaka 20011.
Pambano hilo  alipambana mpiganaji wa Kick Boxer kutoka nchini Kenya Rukia Nachirite, na kufanikiwa kuchukuwa ushindi wa Afrika Mashariki na kati.
Ushindi huo anasema uliweza kumwongezea umaarufu mkubwa, kwa wapiganaji wa kike wa  Afrika na duniani kote kutokana  namchezo wa ngumi.
“Niliweza kujulikana kiasi cha kuanza kupata mwaliko, kwa mabondi kutoka Afrika Kusini” anasema.
Miongoni mwa mwaliko ni kutoka kwa mpiganaji  wa Kickboxer, kutoka Afrika Kusini,  Farasi Coat, ambaye pambano hilo lilimpaswa Pendo kutetea mkanda wake wa Afrika Mashariki na Kati.Farasi Coat  alikuja nchini, alijitahidi ndipo kwa mara ya pili akafanikiwa kubaki na mkanda, na ndipo ukawa mwanga wa kuchaguliwa kwa kuletewa barua kutoka Japan.

“Nilitumiwa barua ya mashindano ya ligi ya K One, yanayofanyika Japan kila mwaka, nikawe miongoni mwa washiriki wa mapambano hayo” anasema.
Lakini Pendo anasema hali ilikuwa tofauti pale alipohitajika kuwa na fedha kama 15 au 20, kuweza kukidhi safari yake hiyo kwa kukaa katika nchi hiyo kwa muda wa mwezi mmoja na ghalama zingine ndogo ndogo.
“Nilianza kutafuta fedha lakini nilishindwa kabisa, kutokana na ushirikiano mdogo wa kimichezo” aliendelea kusisitiza,
Hapo ndipo alipoanza kukutana na vituko, baada ya kuamua kwenda kwenye maofisi ambayo yamekuwa akiamini yanauwezo wa kumdhamini.
Anasema wengi wakajitokeza kuanza kumwekea ahadi ya kumchangia kwaajili ya safari hiyo ambayo ilianza kuonyesha nuru ya mafanikio katika mchezo wa ngumi kwa upande wa Wanawake Tanzania.
Ulifika muda wa kufuatilia ahadi, anasema hapo ndipo vituko vilipoanza kwa kuitwa kwenye hoteli kubwa na kuwekewa mitego. “Mtu ulikuwa unamheshimu, anakupigia simu uende kwenye hoteli ili  akakupe hizo fedha, tena anakwambia  yupo kwenye kikao. (Endelea kusoma ujue cha zaidi)

Lakini ukifika huko, anakuambiwa njoo kwenye chumba namba fulani. Na ukienda unamkuta na taulo, na kukuambia kama unataka fedha ulale naye kwanza’Ufanye mapenzi’ ” anasema Pendo.
Ukikataa anakuruhusu uondoke bila ya kukupa saidia  chochote, jambo ambalo lilizidi kumkatisha tamaa.
Anasema kila alipojaribu kwenda kuomba masaada kwaajili ya kusafiri, lakini ilishindikana kwakuwa tabia ilikuwa ile ile ya kumuhitaji kimapenzi kwanza, harafu msaada baadaye.
“Nikaona siwezi kukubali kuchezewa, ndipo nikaghaili hiyo safari na kuamua kujishughulisha katika masuala mengine madogo madogo” aliendelea kusema.
Lakini hata hivyo mwaka 2012, alitumiwa barua nyingine katika mashindano hayo. Ndipo akaamua kufanya kazi kama promota au mwaandaaji wa mapambano ili kuweza kukusanya fedha kwaajili ya safari.
Miongoni mwa mapambano ambayo aliyaandaa ni ya Kasema na Oswad Maneno, ambalo la kwanza Kaseba alishinda lakini mpinzani wake alikataa.
Pia akaandaa pambano la marudiano, kati ya mahasimu hao wawili. Lakini baadaye tena akaja kuandaa pambano la Rasikosi Mwanza wa Malawi, ambapo alipigwa katika raundi ya tano lakini mapambano yote hayo hakuweza kufikia fedha iliyohitajika na hatmaye akabaki tena bila ya kwenda popote.
“Sasa niliona mchezo wa ngumi hauna faida kwangu, kwakuwa nimeambualia umaarufu” anasema
Anasema tangu aliapoanza ngumi mwaka 2002, hakuna mafanikio yeyote aliyoyapata.
Pendo anasema histori yake ya kupigana ilianzia shule ya msingi hadi sekondari, kwa kupigana na vijana wa kiume kiasi cha kuanz kumuogopa. “Nilikuwa nikipigana na mwanaume, nilikuwa nakunja ngumi na kama mzembe mzembe alikuwa lazima nimwangushe. Watu niliokuwa nasoma nao walivyosikia nimekuwa mpiganaji hawakushangaa” anasema.
Anasema kipindi hicho alikuwa akisoma shule ya msingi Olong’adida iliyopo Manyara, ambapo baadaye akafauru katika shule ya sekondari ya Gallapo day iliyopo Manyara hapo hapo.
Baada ya hapo alianza kutafuta maisha, hadi kufikia kuja Dar es salaam kwa ndugu zake na kuwaacha wazazi wake mkoani Manyara.
“Sisi ni watu wa Moshi, lakini kama unavyotujua wachaga tunahama mikoa kwaajili ya kutafauta fedha” alisema.
Baada ya kufika Dar es salaam ndipo aliapoanza kuweka nia yake ya wazi kutaka kujiunga na mchezo wa ngumi, ambapo rafiki zake wa karibu waliweza kumfikisha hadi kwa Japhet Kaseba, bigwa wa mchezo wa Kick Boxer dunia.
Mwaka 2002 alianza rasmi mazoezi, katika pwani ya Coco Beach akiwa na mpiganaji Kaseba, na baadaye akaanza kupigana katika mazoezi.
“Lakini baadaye Kaseba alikuwa anasafiri, ikabidi anikabidhi kwa Master Kinyogori” anasema Pendo.
Wakati alipofika kwa mwalimu huyo wa ngumi ya Boxer, alianza kujifunza boxer. Anasema mwalimu huyo kwanza alimuona kama msichana mrembo,  lakini alipoanza kumjaribu na wanaume ndipo aliposhituka akiwapiga.
“Alianza kuniamini baada ya kuwadondosha wanaume ambao yeye alikuwa akiwaamini’ anasema.
Ndipo nikaanza mazioezi rasmi kama KickBoxer, ambapo mwaka 2008 nikapigana pambano langu la kwanza na Rehema Chande.
“Niliweza kushinda kwa pambano langu la kwanza, jambo ambalo lilinifanya kuchukua mkanda w mpiganaji bora wa Tanzania” anasema.
Aliweza kushinda pambano hilo kwenye raundi ya 5, akiwa na point 3 na kufanikiwa kuchukua mkanda wa ngumu wa Tanzania upande wa wanawake.
Anasema mkanda huo ulitolewa na chama cha ngumi cha Ufaransa, kilichokuwa kikiitwa World Kickboxer Network (WKN).
Baada ya hapo akaja kupigana tena katika pambano la Boxer, na Flora Malichela, mwaka 2009 Octoba ambapo napo alishinda.Baada ya hapo ndipo nikapata pambano la kupigana na Rukia Machirite, kutoka Kenya katika ubigwa wa Afrika Mashariki na kati, ambapo ulikuwa mwaka 2011.
“Pambano hilo nilifanikiwa kushinda na kuapewa barua ya kwende kwenye mapambano ya K One, Japani” anasema.
Baada ya kutopata maendeleo yoyote, ndipo mfanyabiashara Dotnata Posh, aliamua kumchukuwa na kumuingiza kwenye filamu.
“Napenda sana kumshukuru Dotnata, ambaye alinishauri niachane na ngumi na baadaye kunipa nafasi katika filamu” anasema.
Anasema kwa sasa anashafanya filamu ya Bongo Mafia, ambayo ameigiza na wakali wengi wa mchezo wa ngumi, kama Japhat Kaseba na Mchumia Tumbo.
“Nimeweza kuwa na fikra mpya, baada ya zamani kushindwa sasa hivi lengo lipo kwenye filamu’ anasendelea kusisitiza.
Anasema kutokana na kila sehemu kujaa ngono, hivi sasa ameamua kujipatia ridhiki kwa kuwafundisha wakina mama, ambao wameshindwa kwenda kwenye mazoezi na kuomba wafundishwe nyumbani kwao.
Anasema huwa analipwa fedha kwa kuwafundisha mazoezi, au kuarikwa kwenye Gym, kwaajili ya kuwafundisha watu.
“Kwasasa sina uwezo wa kuanzisha Gym, langu ila ningepata uwezo hata watu wa kunikopesa basi ningefungua na kumlipa kutokana na kile kiingilio”  anaelezea.
Pendo ni mtoto wa tatu, kati ya watoto nane ambapo  mkubwa wao ameshafariki.
Kwa mara ya kwanza wazazi wake waliposikia anacheza mchezo wa ngumi, walimuonya kuwa makini lakini hawakuweza kumzuia sababu tayari walishaona dalili tangu mwanzo.
Mwisho.


Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi