Saturday, July 27, 2013

Gomesa Tv

Kiswahili, Kiengereza bado utata filamu za Kibongo



Naweza kusema kwa sasa soko la filamu limetanua,  ingawa zipo baadhi ya filamu hizo zipo zenye ubora wa kuridhisha na  baadhi yake zimeendelea kuwa tatizo kutokana na mpangilio mbovu wa filamu zenyewe au stori.
Hilo sio tatizo sana ila kubwa zaidi ni katika suala la utumiaji wa majina ya filamu mengi yao kuwa ya lugha za kiengereza, ambapo ndipo ilizaa makala hii.
 Majina mengi yamekuwa yakija kwa mtindo wa Lugha ya Kiengereza, husasani filamu zinazotoka hivi karibuni zikiwemo Imposible, God Promise, Ghost Calamities na nyingine kibao, Before Wedding, Apple na zingine nyingi.
Kabla sijaanza kuulizia zaidi chanzo cha kuingia kwa majina ya kiingereza kwenye tasnia ya soko la filamu Tanzania, nilijaribu kudadisi ni nani wa kwanza kutumia jina la filamu la kiengereza.
Lakini baadhi ya wadau wa tasnia hiyo, ambao ni wateja wa kasi hiyo ya sanaa wengi walisema kwamba, kuibuka kwa nguli wa tasnia hiyo marehemu Steven Kanumba na swahiba wake wa karibu Vicent Kigosi ndiyo mwanzo wa kuibuka kwa filamu za lugha ya kigeni.
Mmoja wa Watanzamaji wazuri wa filamu za kitanzania, ambaye jina lake hakutaka litajwe, alisema Kanumba alifanya hivyo kutokana na kuwa na malengo ya mbali na filamu zake, na ndiyo maana alifanikiwa kufikisha soko la filamu zake mbali.



Alizitaja baadhi ya filamu ambazo alifanya marehemu Steven Kanumba, ambazo zilitumia majina ya kiengereza ni kama Off Side, Uncle JJ, This Is It na zingine kibao.
Lakini hata hivyo swahiba wake Vicent Kigosi ‘Ray’ naye alikuja na filamu kama, Family Diserty, Hot Friday, I hate My Birthday, Danger Zone na nyingine kibao.
Hata hivyo utumiaji wa lugha hiyo katika filamu za kitanzania, wasanii wenyewe wamekuwa na mtanzamo tofauti tofauti, na baadhi ya wasanii na wadau wa tasnia hiyo walieleza mitazamo yao.
Nyota wa filamu nchini, ambaye alishatengeneza filamu kama Tifu la Mwaka, Shahaada, Toba, Fungate, Suria, Issa Musa ‘Cloud 112’, yeye alisema anaona ni kama ulimbukeni wa kutumia lugha za kigeni.
Ingawa anaona huenda mtu akawa anafanya hivyo kutokana na maslahi yake binafsi.
Cloud 11 anasema yeye ataendelea kutumia majina ya lugha ya Kiswahili, katika kuhakikisha anaendeleza utamaduni wa lugha hiyo.
Lakini mwigizaji nguli, ambaye aliibuka na filamu kama Miss Bongo, Kijogoo, Sweat Lie, huku akishirikisha katika filamu kama Red Card, Sobbing Sound, Haji Adam ‘Baba Haji’.
Baba Haji ambaye ni muhitimu wa sanaa ya filamu ya jukwaani,  anasema kutumia lugha ya kiengeleza au ya kigeni ni kulenga soko la kimataifa.
Anasema hata hivyo ni vizuri watu wanaotumia lugha ya kiengereza au ya kigeni yoyote, kuweka na tafsiri ya jina la filamu hiyo.
“Ni bora kutumia lugha ya kigeni na kutafsiri Kiswahili kwaajili ya soko la  ndani” anasema.
Anasema siku moja wakati yupo kwenye kazi zake za uigizaji nchini Zambia, alikuwa akilalamikiwa kwamba kila kitu Kiswahili, jambo amblo wengine wanazipenda filamu lakini wanashindwa kuzielewa.
“Lakini pia tunapotumia kutafsiri  filamu , tuna mpa mtu kazi ya
kufuatilia filamu, na kufuatilia mikasa” alisema.
WWakati huo mmiliki wa kampuni ya Bulls, inayojihusisha kutengeneza filamu nyingi za hapa nchini, pia mwongozaji wa filamu mbalimbali, Single Mtambalike.
Anasema katika filamu zake zote, filamu ambazo ametumia lugha ya kiengeleza ni mbili, Gent Men, na The Stranger, lakini zilizobaki zote ametumia majina ya Kiswahili, kama Uyoga, Swahiba ,Chaguo Langu ,Tamaa Yangu,Jesica ,Mtaani Kwetu ,Kimya .
Anasema yeye huwa analenga sana soko la Tanzania hususani kwa watu wa mitaani, ambao elimu yao haipaswi kuhakikiwa sana kwa lugha ya kigeni.
“Kama filamu zangu nategemea kwanza soko la ndani, sioni sababu ya kutumia lugha ya kigeni” alisema.
Anasema huwa anatumia lugha ya kiengeleza kama kutafsiri, yale yanayosemwa ndani ya filamu lakini jina la filamu linabaki kuwa la Kiswahili.



Kwanza alieleza wazi dhumuni la shirikisho, ambalo ndilo lenye mamlaka ya kusimamia kazi za wasanii wote Tanzania.
Anasema lengo la shirikisho kupambana na maadili, ikiwemo utumiaji wa lugha, mavazi na mambo mengine.
Hata hivyo anasema hali hiyo imekuwa kazi ngumu kutekelezeka kutokana na shirikisho kuandamwana na mambo mengi ya kufanya.
Kwa upande wa kampuni yake anasema kutumia lugha ya Kiengereza katika filamu zetu, kunatokana na soko la ndani lenyewe kuhitaji hivyo.
Miongoni mwa wasanii ambaye naye alitoa maoni yake ni, mwigizaji aliyewahi kuwa mwanamitindo, Yusufu Mlela ambaye tayari alishatoa filamu zake kama Angel, Poor Mind.
Kwa upande wake anasema kufanya filamu za Kiswahili na kuweka jina la Kiengereza,  ni kukuza soko la kimataifa.
“Ni vizuri kutumia Kiengereza, lakini chini kutafsiri Kiswahili ndiyo inapendeza zaidi” anasema.
Anasema kwasasa watu wanalenga zaidi soko la nje, ambapo watu wengi hawajui Kiswahili. Hivyo wanatumia lugha ya kigeni, ili kuwavutia watu ambao hawajui Kiswahili.
Msanii wa kike, ambaye kwasasa huenda ndiyo akawa msanii pekee wa kike aliyeigiza filamu nyingi, Chuchu Hansi aliyetengeneza filamu ya Two Face, na Laura.
Anasema filamu ya Kiswahili kuweka jina la kiengeleza, kunatokana na stori yenyewe ya filamu.
Anasema hata hivyo kutoka moyoni kwake anatamani sana filamu kuwa na majina ya Kiswahili, ili kukuza lugha yetu.
“Tusiwe dhaifu sana katika hilo,  Kiswahili kimekamilika ni bora kutumia zaidi lugha yetu” anasema.
Miongoni mwa wadau wa filamu waliotoa maoni yao, ili kujua ni vema kuendelea kutumia majina ya Kiengereza katika filamu za Kiswahili, ni Makamu mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, pia ni Pia ni mkurugenzi wa Bajomba Film Distibuters, na mjombe wa shirikisho la filamu Tanzania ‘TAFF’ Makame Juma Bajomba.



Bajomba anasema hata katika maisha ya kawaida, Watanzania wenyewe, wanapenda kuchanganya lugha ya kiengeleza na Kiswahili.(Pata utamu zaidi)


“Ujue ukitumia lugha ya kiengeleza, watu wanataka kujua linamaana gani zaidi. Hivyo watu wanajikuta wakinunua ili kuweza kujua zaidi” anasema.
Anasema hata hivyo lazima wasanii waamke na kutumia lugha za asili, katika kukamilisha filamu za Tanzani, ili kuweza kuwavutia wageni.
“Mbona kuna filamu kama Gawa au Odama, zimefanya vizuri tena zimetumia lugha ya kiasili” anasema.
Mwandishi wa gazeti la Habari leo, na Mchambuzi wa filamu Beda Msimbe, yeye alifafanua zaidi kwa kusema.
Jina huwa si tatizo sana kwenye filamu, kutokana na jina sio hali harisi ya filamu yenyewe.
Anasema utumia jina la kigeni, ni sahihi kwakuwa hata nchi zilizoendelea pia hutumia lugha ambazo zisizozilizomo ndani ya filamu yenyewe.
“Zipo filamu nyingi ambazo majina yake sio kilichopo ndani, wala hayaendani na lugha ya nchi husika” anafafanua.
Akitolea mfano wa filamu kama Matrix ambayo asili yake ni mahesabu, lakini filamu haihusiani na mahesabu kabisa.
Aliendelea kutaja baadhi ya filamu, ikiwemo Terminater, na zingine ambazo hutumia majina ambayo hayaakisi picha yenyewe.
“Cha msingi watu huangalia soko, na sio kuangalia jina lina asili ya wapi, na linamaana gani” anaendelea kufafanua.
Mwisho.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi