Thursday, February 14, 2013

Gomesa Tv

Walter aja na makubwa 2013
Mshindi wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, Walter Chillambo, ameachia ngoma yake mpya iitwayo ‘ Siachi’ ambayo imekuwa inasubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wake.
Wimbo huo, ambao baadhi ya mashabiki waliusikiliza kwa mara ya kwanza kwenye tamasha la After School Bash, ameurekodia katika studio za Surround Sound Studios.
Akizungumzia wimbo huo, Walter amesema anaamini utakuwa mkali kwani amefanya aina ya mziki ambayo inawagusa watu wa rika zote na ameutoa maalumu siku ya leo kuwaonyesha mashabiki wake kuwa anawapenda.
 ‘Siachi ni wimbo ambao nimeuandaa maalumu kwa mashabiki wangu ili kuwaonesha hawakukosea kunipigia kura ili niwe mshindi wao’ alisema Walter.
Mkali huyo wa sauti anauzindua wimbo wake ho leo katika Club Maisha ya Dodoma, katika show ambayo inatajwa kufunika mkoa huo.
Walter anasema mpaka sasa ashaanda nyimbo kumi, na mashabiki wajiandae kwani atazidi kuachia nyimbo zaidi hivi karibuni.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi