Saturday, February 16, 2013

Gomesa Tv

Mpoto kuinua sana ya jukwaani Tanzania

(Msami mwalimu wa THT kulia, akija kujifunza mchezo wa jukwaani)
Katika kuhakikisha wasanii wa mchezo wa jukwaani unaendelezwa Mkurugenzi wa Cloud Media Luge Mutahaba, amesema amejitolea kuhakikisha kwamba mchezo huo unapanda chati na kuweza kurudi katika kiwango chake kama ilivyokuwa zamani. Hata hivyo mwigizaji Mtanzania, ambaye aliungana na wakenya saba Mrisho Mpoto alisema haamini kama Watanzania wanaweza kukubali na kuunga mkono mchezo huo ambao umekuwa na radha nzuri. Hata hivyo alianza kuingiwa na moyo baada ya waalikwa wachache kufika kwenye jumba la sanaa lililopo Oysterbay, kuja kushuhudia na kusema watakuwa mabalozi wazuri juu ya kusambaza ujumbe huo. Miongoni mwa waalikwa waliokuwepo hapo ni, Dinamarios, Mh Zitto Kabwe, wasanii wa THT, na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja walikuja kuonyesha imani na kuunga mkono wa matamasha ya aina hiyo.

 Wasanii wa Kenya wakiongozwa na Wanyama na Mrisho Mpoto waliweza kuonyesha vizuri uwezo wao, na hizi ni baadhi ya picha za mchezo huo ambao kwa siku ya jana usiku waliweza kuongeza mashaisha yetu kwa kucheka tena kucheka sana bila ya mpaka.
Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi