Monday, January 28, 2013

Gomesa Tv

Wasanii washikiria msimamo wa kuandamana nchi nzima

 Wasanii wa filamu leo walikuwa kwenye kikao maalum kwaajili ya kuendelea kujadilia masuala ambayo yameendelea kuikumba tasnia hiyo, katika kudai haki yao ya kumiliki kazi zao, na kuomba baadhi ya viongozi katika Bodi ya filamu Tanzania kuweza kuachia ngazi kutokana na kuwa kikwazo katika kutafuta haki zao. Wasanii hao walisisitiza kama hawatapata nafasi nzuri ya kuweza kukaa pamoja na waziri na kumweleza mambo yao, basi wataanzaisha maandamano makubwa ya nchi nzima kuhakikisha baadhi ya viongozi wa Bodi ya Filamu wakitoka.
(Adam Kuambiana akisikiliza kikao)
 Baadhi ya wasanii walitaka wasanii wenyewe kwa wenyewe kwanza lazima waadabishane ilikuweza kuonyesha kwamba ufuatiliaji wa mambo yao yanakuwa ya kiuhakika na wa kufuata sheria kama inavyotakiwa. Hata hivyo baadhi wengine walidai kwamba, wapo wenzao wamekuwa kikwazo kwa kutofika katika kikao hicho, na kusababisha kuzoletesha nguvu ya mapambano dhidi ya maadui zao.
 Nikita Cloud 112 akito maoni yake.
 Adam Kuambiana akitoa mapendekezo yake

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi