Tuesday, January 1, 2013

Gomesa Tv

Siku 10 Sajuki alizimalizia Muhimbili kabla ya kufariki

 Nyota wa filamu na maigizo nchi Juma Kitoloko 'Sajuki' amefariki dunia leo saa moja kasoro, katika Hospitali ya Muhimbili alipolazwa kutoka na maladhi yanayomkabili kwa muda mrefu. Ndugu wa Stara alisema Sajuki alilazwa Hospitalini hapo siku kumi kabla ya kupatwa na Mauti, huku hali yake ikiwa tete kisi.
(Sajuki akiwa na Mwanaye)
 Sajuki amefariki dunia wakati akiwa kwenye mpango wa kutafuta fedha kwaajili ya kurudi tena nchini India kwaajili ya matibabu ambayo mwanzo alipelekwa na kurudishwa na kuambiwa apelekwe tena.
 Hata hivyo siku moja Sajuki aliwahi kusema kwamba muda wa kurudi India, ulikuwa umeshafika na kuanza kupita lakini fedha za kwenda kupata matibabu hayo zilikuwa bado hazijatimia jambo ambalo lilimfaanya awe anafanya matamasha ambayo yangemwezesha kuongeza fedha kidogo kwaajili ya kurudi tena India kupata matibabu.
BONGO UNIT..... Inawapa pole Familia ya Sajuki, na Familia ya Wastara akiwemo na Wastara mwenyewe, pia inawapa pole Wasanii wote, pamoja na Watanzania . BWANA AMETWAA NA BWANA AMETOA........

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi