Friday, January 18, 2013

Gomesa Tv

Mkutano wa TAFF wamwimbia wimbo Jk

 Shirikisho la wasanii Tanzania 'TAFF' leo limefanya kikao ili kuweza kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuendesha shirikisho hilo, kutokana na upungufu wa fedha walizokuwa nazo. Raisi wa shirikisho hilo Simon Mwakifamba, alisema shirikisho hilo halitegemei fedha kutoka Serikalini hivyo ni juhudi zao pekee ndizo zinazoweza kufanikisha kwao. Alisema pia sheria mbalimbali zimekuwa zikiwabana, hivyo huu ni wakati wa wao kuungana na kushikamana ili kuweza kupamba juu ya ufisadi wanaofanyiwa, kwenye tasnia yao kuanzia kwenye sheria ambao inawapa nafasi kubwa Wasambazaji kuwa na haki.
 Mwakifamba pia alitaka wasanii kuichangia Shirikisho hilo kwa moyo mmoja ili kuweza kufanikisha huku akitoa tamko kwamba anaimani na raisi Kikwete juu ya kupamba nao na kuwasaidia katika kusaidia. Hata hivyo jambo ambalo lilianza kuwashangaza wengi katika kikao hicho kilichofanyika Vijana Kinondoni, pale raisi huyo wa shirikisho alipoanza kuwaimbisha nyimbo za kumsifu Kikwete.
 Wengi tukio hilo liliwasononesha na kusema kwamba huo si wakati wa kuimba na kumsifu mtu, kwani ni muda wa kupambana na kuangalia haki zao, kwakuwa raisi ni wajibu wake kupamba na kulinda masilai ya watu wake. Mmoja wa wasanii alisema haoni sababu ya mkutano huo kuendeshwa kisiasa, kwani kuanza kuimba nyimbo za kumpongeza mtu.
 Dr Cheni akiwa na Dino
 Steve Nyerere

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi