Wednesday, January 9, 2013

Gomesa Tv

Hivi ndivyo alizikwa Omari Omari

Mwanamuziki aliyetamba na wimbo wa Mchiriku, Omari Omari aliyefariki dunia hivi karibuni leo amezikwa kwenye makabuli ya Mikoroshini Temeke na wasanii na watu wengine. Katika mazishi hayo yaliudhuru na baadhi ya wasanii wa filamu na muziki, huku watu wakihoji kwanini wasanii wengi hawakuwepo jambo ambalo wameamini kwamba huenda wasanii wamekuwa na ubaguzi juu ya nani wa kumzika nani wa kumwacha
 Miongoni mwa wasanii ambaye alijitolea sana katika msiba huoni Saidi Fella, ambaye yeye alikuwa mstari mbele kuhakikisha shughuli hiyoinaisha salama. Hata hivyo balaa la eneo hilolilikuja wakati wa kuzika, kwani vurugu zilikuwa nyingi kiasi cha watu kuhofia usalama wa mali zao na kukaa pembeni baadaha ya kuonekana uhuni ukiwa mkuba.
 Hata hivyo wasanii pia walijitokeza ingawa si kwa wingi, ila baadhi yao alikuwepo Dr Cheki, Mzee Yusufu, Ali Jay, Juma Nature Chege, Dully Syskes, Waziri Ally, Inspector Haroon na wengine ambao walikuja kumsindikiza msanii huyo aliyetamba kwa muda mfupi.

 Dk Cheni akiwa na mzee Yusufu
 Juma Nature akiwa ametulia pembeni.
 Inspecta Haroon akiwa kwenye pozi na mwanamuziki wa Mabaga Freshi.
 Wawakilishikutoka TAFU, raisi wa wawasanii Mwakifamba na mwakilisha kutoka Bongo Movie Chiki MchomaGomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi