Tuesday, December 11, 2012

Gomesa Tv

Unajua kwanini wasanii wanawaogopa waigizaji wa nje?Mwigizaji  ‘Dk Cheni’ amekiri  mauzo mabaya ya filamu yake ya My Flower lilimfanya abadili sokola filamu na kuingia vichekesho.  alisema alikuwa na desturi ya kuulizia kila kazi zake zinazoingia sokoni, lakini alipoulizia kuhusu kazi hiyokwenye maduka aliambiwa wazi kwamba imedorora.
Alisema tatizo hilolilimuumiza sana kichwa, mpaka kuamua kuirudia kuingalia mara mbili mbili hadi alipoamua kubadilika na kuanza kufanya filamu za vichekesho ‘Comedy’.

Miongoni mwa filamu za vichekesho alizofanya ni Dhuluma, Return Love, Dk wa Kifimbo na Majanga.
Pia Dr Cheni alieleza sababu ya  wao kushindwa  kumudu soko la kimaifa, kunatokana na  gharama kuwa kubwa  za kuwaita  wasanii wa nje wakati kipato chao kipo pale pale.
Alifafanua zaidi kwa kusema kwamba  wasanii wanatamani  kuigiza na wasanii wakubwa kutoka nje kama Nigeria na Ghana, lakini kutoka na gharama kuwa kubwa za kumleta msanii, hata hivyo wakipeleka kwa  Msambazaji  hulipwa fedha zile zile za kawaida.
Dk Cheni alisema Msambazaji hatizami umetumia kiasi gani katika kazi hiyo, anachojali yeye kukupa kile kiasi chako hata kama atauza mapato makubwa zaidi.
Alisema jambo hilo limekuwa likiwakatisha tamaa, na kuona haina haja ya kuingia gharama kuwaleta wasanii wa nje  wakati wanachopata ni kile kile cha siku zote na kuwafaidisha wengine.
Aliendelea kwa  kusisitiza na kusema ,  wanachowaingizia wasambazaji ni kikubwa  kulikokile wanachopewa na wanashindwa kufanya lolote sababu wasambazaji wanahaki kubwa.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi