Tuesday, December 11, 2012

Gomesa Tv

Kizazaa cha uongozi mpya Bongo MovieMWIGIZAJI  nyota  wa filamu nchini Vicent Kigosi ‘Ray’, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Bongo Movie, baada ya kushinda kwa kura 53 kati ya 54 huku akiahidi kupambana na waandishi wanaowadhalilisha wasanii wa filamu.

 
Akizungumza katika kikao  baada ya kushinda kiti hicho, alisema hatofumbia macho  waandishi wanaojaribu kupotosha ukweli juu ya mambo mbalimbali yanayowahusu wasanii wao.
Pia aliendelea kwa kusema atapambana na wasanii ambao wamekuwa chanzo cha kuvuja siri za ndani kabisa za wasanii wenzao kwa kwenda kuuza stori kwa waandishi.


“Tunawajua wanaokwenda kupeleka stori kwa waandishi na kuwachafua wenzao, lakini safari hii hatutokubaliana nao” alisema.
Ray alisisitiza kupambana na mahojiano ya uchochezi kwa mtu kuhojiwa upande wa kwanza na upande wa pili kuhojiwa mwenzake na kuwatengenezea bifu bila kujijua.
Miongoni mwa wasanii wengine waliochaguliwa katika kamati hiyo, ni Jackline wolper, Irene Uwoya, Single Mtambalike.
Wakati huo msanii Jacob Stephan, yeye ndiyo aliyekuwa akimalizia muda wake na kumwachia Ray, kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mwingine.


 Huu ndiyo uongozi mpya wa Bongo Movie,  Jack Wolper, Vicent Kigosi, Rado, Single Mtambalike, Irene Uwoya na wengine.
 Vicent Kigosi mwenyekiti mpya wa Bongo Movie
 Jack Wolper mweka azina msaidizi
 Richie rich mweka azina wa Bongo Movie
Shemsa Ford akitoa changamoto chake juu ya uongozi ujao

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi