Tuesday, December 11, 2012

Gomesa Tv

Hii ndiyo furaa ya Wema kwa sasaNYOTA  wa filamu nchini Wema Sepetu , amesema kutoonekana kwake kwa watu kunampa furaha na faraja kwakuwa alishachoka kutajwa tajwa midomoni mwa watu.

Wema alisema  kuulizwa  mbona siku hizi haonekani na wasanii wenzake kuna mpaimani kwamba hapatikani ovyo jambo analohitaji liwe hivyo siku zote.
Alisema kwa  sasa kila kitu atakuwa akifanya kwa siri, kutokana na kuamini  umaarufu si kila kitu chako kiwe wazi kwa wengine, kama ilivyokuwa zamani.
“Nafurahi sana ninapoambiwa mbona sionekani, na wengine wanaponitafuta na kunikosa” alisema
Wema alisema hata safari zake za ndani na nje ya nchi, zote zitakuwa siri, na wala  hataki kitu chochote kinachomhusu yeye kuwa nje.
Aliendelea kusema hivi sasa atakuwa akifanya kazi zake zote kimya kimya, akiamini huo ndio umaarufu ambao anautaka na sio wa kuweka wazi mambo  hadi ya siri.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi