Tuesday, December 25, 2012

Gomesa Tv

DJ Topspin kutoa burudani Club 327 Usiku wa Mwaka Mpya

Club 327 leo imetangaza kuwa DJ Topspin wa Marekani ndiye atakayekuwa kwenye moja na mbili kuwapa burudani wote watakaohudhuria Club hiyo katika kusherekea usiku wa Mwaka Mpya. DJ Topspin amekuwa kipenzi cha watanzania wengi, tokea alipokuja kwa mara ya kwanza mwaka uliopita katika sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya Groove Theory hapa Dar es Salaam.

Mmiliki wa Club 327, Lawrence Kadri, alisema uwepo wa DJ Topspin siku hiyo ya mwaka mpya unaifanya Club 327 kuwa sehemu pekee ya wapenda muziki wa jiji la Dar es Salaam kuja kufurahia. ‘Sisi Club 327 tunaamini katika kuwapa wateja wetu upekee katika soko, na ndio maana tumeifanya Club hii kuwa sehemu maalumu kwa wapenda muziki wote’ alisema Kadri.

‘Kama mnavyojua, msimu huu wa sikukuu sehemu mbalimbali zimekuwa zikiwaandalia wateja wao vitu mbalimbali, lakini sisi Club 327 tumeandaa burudani kwa watu ambao watapenda kusherekea siku ya mwaka mpya stejini’ alisisitiza Kadri.  DJ Topspin anasifika kwa uwezo wake wa kucheza nyimbo za aina mbalimbali ikiwemo Top 40, Hip-Hop, Old School, Soulful House, Reggae lakini pia umahiri wake wa kuwapa wasikilizaji vionjo tofauti wawapo stejini.

Huku mtindo wake ukijulikana zaidi kama “Cognac-Smooth”, DJ Topspin pia atapata nafasi ya kusalimiana na baadhi ya wageni waalikwa ukumbini hapo watakokuwa kwenye chumba maalumu cha Hennessy.  Tanzania ni mojawapo ya sehemu ambazo DJ Topspin anazikubali kama sehemu za burudani ambapo anasema, ‘Tanzania ni nchi ambayo ina nafasi kubwa katika moyo wangu, ikiwa ni nchi pekee niliyoitembelea Afrika ambayo imebadilisha mtazamo wangu kuhusu bara hili’ alisema Topspin.

Sherehe za Mwaka Mpya zitaanza rasmi saa tatu kamili usiku tarehe 31, huku DJ Topspin akitarajiwa kuanza kutoa burudani muda kidogo kabla ya saa sita usiku hadi asubuhi, kiingilio kikiwa ni shilingi elfu 30,000/-.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi