Monday, December 31, 2012

Gomesa Tv

Asha Baraka akutananisha wanafamilia Leaders Club

 Mkurugenzi wa ASET na mmiliki wa Bendi ya Twanga Pepeta jana amefanya bonge la Tamasha la kukata na shoka kwaajili ya kuukaribisha mwaka wa 2013 akiliita kama Family Day. Katika tamasha hilo liliweza kukutanisha wasanii mbalimbali wa fani mbalimbali, wakiwemo wale wa uigizaji na waimbaji wa bendi zingine. Pia kulikuwa na burudani kwaajili ya kuwachangamsha watoto wa lika zote, huku akihitaji wasanii wote kushirikiana ili kuweza kuinua tasnia hiyo
Asha alisema sababu ya kufanya hivyo ni kutaka pia kuonyesha vipaji vya watu wengine, ambao kama wacheza show na waimbaji wachanga ili watu wenye shida na wasanii katika bendi zao waweze kujichukulia .
Asha pia alitoa shukrani kwa wadau wote walioweza kufika eneo hilo kwaajili ya kupata burudani kutoka kwao
Mwanamuziki kutoka Mapacha Watatu, Jose Mara naye alikuwepo kwaajili ya kujumuika na wanafamilia wa Twanga.
Wasanii wa Bongo Movie, kulia ni Mr Kupa, Steve Nyerere na Saguda.
Wanamuziki wa twanga Pepeta, Kulia ni Haji Ramadhani mwimbaji wa Twanga Pepeta na mshindi wa Bss 2011, wa kati ni Alex mtoto wa Steve Nyerere na mwingine ni Mnenguaji wa Twanga.

Mkongwe wa Twanga pepeta
Mkwabi akiwa na Dokii wakiwa kwenye pozi la pamoja, Dokii naye alitoa burudani kali kwa mashabiki wake.
Awadhi kutoka Bongo Movie,
Isha Mashauzi naye alikuwepo kwaajili ya kutoa burudani na Mashauzi Clsassic
Mr Kupa

Steve Nyerere akiwa na watoto wake kwa furaha ya kifamily
Hapa Mr Gomesa naye alikuwepo kwaajili ya kufurahi na wana Twanga.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi