Friday, November 23, 2012

Gomesa Tv

Swahili Hip Hop Summit 2012, yapunguza machungu ya Wanahip hop

 Wasanii mbalimbali wa muziki wa kufoka maarufu kama Hip Hop leo walikutana katika kikao cha wasanii wanaofanya sanaa na muziki wa aina hiyo,  kilichoandaliwa na Asar Entertaiment na Alliance Francaise, katika ukumbi wa Alliance Francaise Hall, ilikuweza kujadili ni jinsi gani wanaweza wakaendeleza sanaa hiyo katika kilele kilichojulikana kama  Swahili Hip Hop Summit 2012. Wasanii walioweza kukutana hapo wengi wao wakiwa ni wale wanaotumia staili hiyo, huku lengo kubwa likitaka culture ya muziki huo kufika mbali zaidi, huku wakiomba uungwe mkono na wadau mbalimbali, ambao wamekuwa wakisimamia muziki hapa nchini
 Pia katika kikao hicho wasanii wa muziki huo hususani kutokea Arusha, waliweza kutoa maoni yao hususani juu ya jinsi ya kupambana na uharamia, huku wakipata taarifa kutoka kwa Wanahip Hop mbalimbali kupitiakatikamtandao wa Sky, ambao nao waliweza kuelezea jinsi ya mapambano ya muziki huo unavyokwenda, hali ambayo iliwapamoyo juu ya safari ndefu wanayoelekea.
Danny Msimamo akiimba  
(G Solo)
 Pi wasanii hao walitoa burudani, ambapo ilionyozwa na Danny Msimamo, G Solo, Mzee Kitime, na
Mapacha, JCB, Saigon na wasanii wengine kibao huku biti ya muziki huo ukipigwa kwa vifaa vya asili na hatmaye kutoa muziki fulani ambao kila mtu alishangaa kuwepo kwa muziki huo. Miongoni mwa watu ambao alitokea kuukubali ni Producer mahiri hapa nchini, Lamar.

 Mzee Kitime, akiandaa hutuba ambayo alitoa maelezo juu ya histori ya muziki, wapi ulipotoka na hapa ulipofikia na hatmaye yake.

 J. C. B Danny Msimamo

 Director wa Asar Entertaiment, Abbas Maunda
 Producer kutoka Fish Crab Record, Lamar
 Mchizi Mox naye alisema doleee. bila ukucha.

Saigoni

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi