Tuesday, November 27, 2012

Gomesa Tv

SHAROMILIONEA KUZIKWA KESHO KIJIJINI KWAO TANGA

 

MSANII nyota wa uchekeshaji hapa nchini, Hussein Mkiete, maarufu kama 'Sharomilionea' anatarajia kuzikwa kesho (Jumatano) huko kijijini kwao Lusanga, Lushoto mkoani Tanga.
Kifo cha mchekeshaji huyo kimegusa hisia za walio wengi, ambapo msanii mwenzake  King Majuto alikimbizwa Hospitali baada ya kushikwa na presha, ambayo ilihatarisha maisha yake pia.
Kwa mujibu wa mtoto wa King Majuto, Hamza Majuto,  hali ya baba yake inaendelea vizuri kutokana na kuumizwa zaidi na msiba wa Sharomlionea anayetamba katika ulingo wa filamu na muziki hapa nchini.
Msanii huyo alikufa jana saa mbili za usiku Maguzoni, kilimita chache na kijijini kwao Lusanga, wilayani Muheza mkoani Tanga, baada ya gari lake alilokuwa akisafiria lenye namba za usajili T478 BVR Toyota Harrier kupinduka na kusababisha kifo chake.
Taarifa za kifo hicho zilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constantine Masawe, na kusema kuwa mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Teule, Muheza, mkoani Tanga kwa taratibu za mazishi zinazopangwa na familia yake.
 
Sharomilionea ameshacheza filamu nyingi za uchekeshaji na kujipatia sifa kubwa, ikiwamo ile ya Sharo Millionea, Imekula Kwako, Jini Mahaba, Porojo na nyinginezo zinazofanya vyema katika tasnia ya filamu nchini.
Wasanii wengi wa tasnia ya filamu na muziki waliozungumzia kifo cha Sharomillionea wakiongozwa na Steve Nyerere, wameonyesha kuchanganyikiwa kwa msiba wa msanii huyo.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi