Tuesday, November 20, 2012

Gomesa Tv

Filamu ya Get Out na maisha ya Kalulu

 Miongoni mwa filamu ambazo zinatoka wiki hii ipo na GET OUT, ambayo imetengenezwa na kampuni ya Nyerere the Power, ambayo iliongozwa na Saguda George huku kamera ikishikwa na Faridi Uwezo. Ni miongomi mwa filamu kali ambazo zimejaa vituko kama kawaida ya Steve Mangele ambaye anatambulika zaidi kwa jina la Steve Nyerere, ambaye alikutana na wakali wengine kama Batuli, Shamsa Ford na Sintah.
 Kila ninapoikumbuka stori ya filamu hii basi nijikuta nikicheka na kusema kweli wabongo sasa upeo unapanuka wa kuweza kufikiria vitu tofauti, ila tatizo linakuja jinsi ya kutoka na kulivaa soko la nje. ndani ya filamu hii ambayo Steve ameigiza kama Kalulu, amekuwa na vituko vya ajabu pale alipogundua kwamba mabosi wake watatu wanaishi kwa kumtegemea yeye, kwakuwa yeye ni kama mlinzi wa nyumbao na mali zao.
 Lakini sio mlinzi wa mali tu, ila madaraka yanazidi kupanda na kumilishwa vitu vingine vya ndani zaidi huku jambo ambalo linampa kibuli mpaka anajisahau kama yeyeni mlinzi tu, na mlinzi kwake ni getini kwaajili ya kufunga na kufungua geti.


 Si filamu ya kukosa, na kama utakosa basi utakuwa umejinyima furaha ya maisha yako,kwakuwa kucheka ni kuongeza siku za kuishi nawe usijizuie kucheka.

Gomesa Tv

About Gomesa Tv -

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :

https://www.facebook.com/gomesamohamedi